HABARI MSETO (HEADER)


 


Breaking

April 25, 2026

KLINIKI YA MAZOEZI RIADHA DAR YAZIDI KUNOGA - MKAPA STADIUM

KLINIKI ya Mazoezi ya Mchezo wa Riadha inayoendeshwa na Chama cha Riadha Mkoa wa Dar es Salaam (DAA), imeendelea tena leo Jumamosi Aprili 25 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa huku ikizidi kuvutia washiriki wengi.



Kliniki hiyo iliyoendeshwa Kocha Amani Ngoka akisaidiwa na David Mabula, ilishirikisha makundi ya umri mbalimbali kuanzia miaka minne na kuendelea, ambapo washiriki walipewa mafunzo ya aina mbalimbali kulingana na umri na aina ya mchezo.


Katika kliniki ya leo, wanafunzi kutoka Shule ya Msingi Toangoma na Sekondari ya Saku, walishiriki kwa mara ya kwanza.



Mwalimu wa michezo kutoka Saku Sekondari, Madamu Johari, ameeleza vijana wake wamehamasika baada ya kushiriki Mashindano Maalumu ya Kusaka Vipaji 'DAA Youth Talent Championship' yaliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.


Kwa upande wake, Kocha Ngoka ambaye pia ni Mwenyekiti wa DAA, alielezea kufurahishwa na mwitikio wa washiriki na kutoa wito kwa wale ambao bado, wajiunge katika programu hiyo inayofanyika kila Jumamosi kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi 5:00 asubuhi.



Ngoka, aliwaomba wadau mbalimbali kujitokeza kutembelea kliniki hiyo kila Jumamosi na kutoa sapoti kwani inakabiliwa na changamoto kama uhaba wa maji ya kunywa kwa washiriki, vifaa kwa washiriki kama viatu, jezi, tracksuits na vinginevyo.

No comments:

Post a Comment

Pages