HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 02, 2019

TMA YATAHADHARISHA MVUA MIKOA 11

Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dk. Agnes Kijazi.


Na Irene Mark

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imewataka wakazi wa mikoa ya Kanda ya Ziwa na jirani kuchukua tahadhari ya mvua kwa siku tatu mfululizo kuanzia leo, Desemba 2, 2019.

Tahadhari hiyo ilitolewa jana usiku na kuitaja mikoa itakayokumbwa na mvua hizo kubwa ni Kagera, Geita, Mwanza, Katavir, Shinyanga, Simiyu, Kigoma, Tabora, Mara, Manyara na Arusha.

Kwa mujibu wa tahadhari hiyo wakazi wa maeneo wametakiwa kusafisha mazingira na mitaro ya maji ili kuruhusu maji ya mvua kutiririka huku wakijikinga na mafuriko.

"Athari zinazoweza kujitokeza ni makazi kuzungukwa na maji, uchelewaji wa usafiri na shughuli za kiuchumi na kijamii," ilisomeka hivyo sehemu ya tarifa ya TMA hivyo lazima kuchukua tahadhari.

No comments:

Post a Comment

Pages