HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 22, 2020

ASILIMIA 40 YA KESI MKOANI KAGERA NI MIGOGORO YA ARDHI-JAJI KAIRO

Mjumbe wa Baraza la Ardhi na Nyumba, Jenesta Rugakingira, baada ya kuapishwa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Marco Gaguti.

Na Alodia Dominick, Bukoba

Jaji Mfawidhi Kanda ya Bukoba, Lucia Kairo, amesema kesi zinazopokelewa mahakamani katika mkoa wa Kagera ni asilimia 40 ya kesi zote zinazopokelewa mahakamani ni
za migogoro ya ardhi hapo.

Jaji huyo Lucia Kairo alitoa takwimu hiyo baada ya kuapishwa kwa wajumbe wateule wawili wa baraza la ardhi na nyumba ambalo litafanya kazi katika halmashauri za Bukoba na Misenyi ambapo walioapishwa ni Annameri Kokuleba na Jenesta Rugakingira


Kairo alisema, utoaji wa haki umejikita katika swala la uaminifu na weledi hivyo wajumbe walioapishwa hawana budi kutenda haki katika kutoa maoni na ushauri mahakamani.

"Baraza watoe maamuzi katika kutoa haki watoe kwa muda stahiki, haki ambayo imecheleweshwa ni sawa na haki ambayo imenyimwa na  haki ambayo imeharakishwa ni sawa na kuwa imezikwa"Alisema Jaji Kairo.

Aliongeza kuwa, haipaswi kuchelewesha haki ya mtu na wala haki isiharakishwe sana kwani humo kuna haki zinaweza kuwa zimemiinywa.

Kwa upande wake, mwenyekiti baraza la ardhi Bukoba na Misenyi Emmanuel Mogasa alitaja takwimu ya migogoro ya ardhi kuwa kwa mwezi wanapokea kesi 966 upande wa Bukoba ambazo zinahusisha mipaka, dhamana benki baada ya wanafamilia kutojadiliana katika kutoa mikopo benk na kukomboa mashamba ya ukoo.

Mogasa alisema, kesi zilizoamliwa mwaka jana zilikuwa zaidi ya 900 na kwa mwezi wanaamua kesi zaidi ya 70 na  wanapokea kesi 60-70 kwa mwezi.

Mmoja wa wajumbe wa baraza la ardhi na nyumba aliyekula kiapoJenesta Rugakingira alisema kwamba, jukumu lao kubwa ni kusikiliza kesi na kutoa maoni au ushauri na kuwa watatoa haki katika kutoa maamuzi yao.

Kwa upande wa Shehe wa mkoa wa Kagera Haruna Kichwabuta aliwasihi wajumbe wa baraza la ardhi na nyumba kutoa uamuzi sahihi kwani ardhi ni tamu hivyo watakumbana na mambo mengi wamtangulize mwenyezi mungu ili awafungulie milango ya ufahamu watoe maamuzi yaliyo sahihi.

No comments:

Post a Comment

Pages