Mkurungenzi
Mkuu wa Shirika la Fedha IFC, Frank Ajilore, akizungumza, na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam. (Na Mpiga Picha Wetu).
NA FARAJA EZRA
BENKI
ya Dunia kupitia kupitia Shirika la Fedha (IFC) na Kampuni ya Mikopo
ya Nyumba Tanzania( TMRC) zaingia Ubia kuendeleza upatikanaji wa mikopo
ya Nyumba za Makazi yenye gharama nafuu.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa
Shirika hilo Frank Ajilore, alisema IFC limewekeza kiasi cha dola za
kimarekani milioni 5. 75 sawa na shilingi bilioni 13.3 kwaajili ya
kuwezesha ukuaji wa soko la mikopo ya Nyumba za Makazi nchini.
Aidha kuwawezesha jamii kupata Makazi bora lakini pia upatikanaji wa Nyumba za Makazi za gharama nafuu.
Alisema
uwekezaji huo unahusisha Shirika la la IFC kununua hisa za TMRC zenye
thamani ya don'tola milioni 1.5 na kuwekeza milioni 4.25
zitakazowezesha Kampuni ya mikopo kutoa hati fungani kwenyev soko la
mitaji kwa muda wa miaka mitano.
Alisema
IFC imejipanga kuwezesha ukuaji wa soko la nyumba nchini kwa
kuwezesha upatikanaji wa fedha ilinkuongeza Kasi ya ukuaji wa soko la
nyumba za gharama nafuu.
Naye
Makamu Mwenyekiti wa bodi ya TMRC Alieleza kuwa TMRC ni Taasisi ya
kifedha iliyoanzishwa mwaka 2010 ikiwa ni moja ya utekelezaji wa mradi
wa Serikali uliofadhiliwa na benki kuu ya Tanzania na iliwezesha mikopo
ya milioni 70 kwa ajili ya kutoa mikopo kwa wateja kupata makazi bora.
Huku IFC ni Taasisi ya kibenki ambayo hujishughulisha na maendeleo ya sekta binafsi kwenye nchi za uchumi unaoendelea.
"
Hadi sasa TMRC imeshatoa mikupuo miwili ya hati fungani yake yenye
thamani ya shilingi bilioni 21.7 na kuioroshesha kwenye soko la hisa la
Dar es Salaam na kupunguza utegemeza kwa pesa za umma" alisema na
kuongeza.
"Uwekezaji huu
wa IFC utawezesha TMRC kuvutia wawekezaji wengine wapya kwenye
hatifungani yake nabhivyo kuwezesha Kampuni ya mikopo ya nyumba kupata
Fedha za muda mrefu" alisema.
Hata
hivyo alisema Uwekezaji huo umejikita katika maeneo mbalimbali
ikiwemo, ujengaji wa uwezo kwenye masoko ya Nyumba , utoaji wa elimu kwa
umma kuhusu mikopo ya nyumba , kujenga uwezo wa benki zinazotoa mikopo
ya nyumba na namba Bora ya kutoa mikopo.
No comments:
Post a Comment