Wanafunzi na Walimu wa Sekondari ya Balang’dalalu Wilaya ya Hanag.
Na Bryceson
Mathias
MKUU wa Wilaya ya Hanang
mkoani Manyara, Joseph Mkirikiti, ameonya Ubinafsi na Siasa za Makundi, ni Msumari
wa Moto uliochelewesha Maendeleo ya Elimu wilayani humo, na kujigamba kupitia
Mchango wa Serikali ya Awamu ya Tano, Elimu sasa inashika Kasi!.
Mkirikiti alisema hayo alipohojiwa
juu ya Kilio cha Wananchi kuhusu Changamoto za Miundombinu Mibovu ya Majengo,
Maabara na Upungufu wa Walimu wa Sekondari Kongwe ya Bweni ya Balang’dalalu
ambayo 2019/2020 Kidato cha Nne na Pili ilifanya vizuri ikiwa na Div 1=14, II=23,
III=19, IV=19, na 0=6, ambapo Mwandishi hakuuruhusiwa kupiga picha ya
majengo hayo kwa madai kuna Katazo!!
Akifafanua alisema, hili si kificho
tangu niingia hapa 2018 kwa msaada wa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), John
Magufuli, na Katibu Mkuu, Ally Bashiru, kazi ilikuwa ni kuvunja makundi ya
kisiasa baina ya, Mary Nagu, na Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye, ili
kuleta Umoja, ambayo yalikwamisha ihata Maendeleo ya Elimu.
“Miongoni mwa wana Umoja wa wana
Hanang in Dar walipotaka kurudi kwao kuja kuchangia Maendelo, walionekana kana
kwamba wanataka kuja kugombea Ubunge au Udiwani, hivyo kile walichokuwa nacho
kwa ajili ya kuchangia maendeleo ya Miundo Mbinu na Elimu walishindwa kuepuka
maneno.
“Tunaishukuru Serikali
kupitia kwa Rais Magufuli, Waziri wa TAMISEMI na Katibu Mkuu wake, walitoa Mil.
115 ambazo zimejenga Hostel na Halmashauri ya Hanang iliyotoa Mil.20 ambazo
zimemalizia ili wakitusaidia tukarabati Mabaara”.alisema Mkirikiti
Diwani wa Kata hiyo, Paulo Tsaxara,
alisema Sekondari ya Balang’dalalu ilikuwa ya Kanisa la Kiinjilili la Kilutheri
Tanzania (KKKT) tangu 1988 ikachukuliwa na Serikali, nakiri Miuundo Mbinu yake
ni mibovu na ina Walimu wachache maana ilisahauliwa, lakini kwa sifa ya ufaulu
iliyonao ikumbukwe!.
“Mbali ya Ubinafsi na Makundi
ya Kisiasa, chnagamoto nyingine ni wenyeji kuona sekondari hiyo kama siyo yao
kwa sababu walipoomba pia iwe na Wanafunzi wa Kutwa ili wenyeji Watoto wao
wasome! Haikukubalika kwa wanafunzi wengi wanatoka nje” alisema Diwani Tsaxara alyesema alisoma shule hiyo ikiwa ya msingi
1973.
Diwani Tsaxara, ameiomba tena
Serikali na Viongozi waliosoma shule hiyo wakiwemo, waliowahi kuwa Wakuu wa
Wilaya nchini, Majaji, Viongozi wa dini ikiwemo KKKT, Waandishi (akimtaja,
Zephaniah Ubwani, na yeye), kuikumbuka shule hiyo iliyo na maabara mbovu na
walimu wachache jiapo wanafanya kazi nzuri, iweze kukarabatiwa maana mabati yake
yenye kuoza ni ya 1988.
No comments:
Post a Comment