Mhandisi wa mamlaka ya mawasiliano nchini TCRA Kadaya Baluhye akiongea
na mafundi wa vifaa vya kieletroniki kwenye mkutano wao na mamlaka hiyo
jijini Arusha. (Picha na Ahmed Mahmoud).
Na Ahmed Mahmoud, Arusha
Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA Kanda ya kaskazini imewataka mafundi wa vifaa
vya kieletroniki ikiwemo simu za mkononi kuwa kwenye mfumo wa umoja kwa
kuanzisha vikundi vyao kwa Kanda au mkoa.
Kwa
muktadha huo kuanzia mwezi julai mwaka huu hakuna fundI ambaye
atafanyakazi kama hajasomo wala kusajiliwa hivyo ni muhimu kwenu
kujiunga kwenye kikundi ili kupatiwa elimu.
Kauli
hiyo imetolewa na Mwanasheria wa mamlaka hiyo Kant Mosha wakati wa
mkutano wa mafundi wa vifaa vya kieletroniki uliofanyika kwenye ukumbi
wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha ambapo aliwataka kuacha kutokuwa na
usajili wa kikundi ndio suluhisho.
Alisema
kuwa mafundi simu ni kada ambayo ilikuwa imesahauliwa hapo awali lakini
kupitia serikali ya awamu ya tano chini ya Rais dkt.John Magufuli
imeamua kuwatambua hivyo kuungana ni sehemu ya kufanikiwa kwa malengo
yenu.
Kwa upande wake
Mwenyekiti wa chama cha mafundi simu Kanda ya ziwa Maguwa Manyanda
amewataka kutambua kwamba mafundi simu ni wathamani kwani jamii
inwategemea na wanachangia mapato ya serikali hivyo busara ni kuona
umoja ndio suluhisho la changamoto zao.
Alisema
kuwa mafunzo hayo yataondoa changamoto na kuwafanya kuwa huru katika
shughuli zao za kila siku hivyo umoja ni nguzo ya kuwafikisha kuweza
kushirikiana na serikali katika masuala mbalimbali ikiwemo vyombo vya
Dola.
Alieleza kuwa
kufanikiwa ili kila moja aweze kutenda kazi zake ni muhimu Sana
wakajiunga na umoja ili kuondoa changamoto zao ambazo zimekuwa
zikiwafanya kujikuta wakikumbana na jeshi la polisi.
Nae
Mwenyekiti wa umoja wa mafundi simu Kanda ya kaskazini Nasri Mshana
Mtengeti alisema kuwa wamefirahi Sana kupata elimu hiyo ya umoja ambayo
itawasaidia kuondokana na changamoto hivyo tuhamasishane kujiunga na
umoja huu.
Awali akitoa
mafunzo kwenye mkutano huo mratibu wa vikundi hivyo kutoka mamlaka ya
mawasiliano mhandisi Kadaya Buluhye aliwataka mafundi hao kufanyakazi
kwenye umoja kwa lengo la kupata elimu na usajili.
Alisema
kuwa jeshi la polisi linafanyakazi ya kulinda usalama na Mali za raia
Ila umoja wenu utasaidia kufanya kazi kwa karibu na jeshi hilo na
kuondoa changamoto zenu ambazo mmekuwa mkikumbana nazo kama mafundi.
No comments:
Post a Comment