Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Lugano Kusiluka, akizungumza wakati wa kongamano la vijana wanaosoma vyuo mbalimbali nchini lililoandaliwa na chuo hicho ambalo linafahamika kama (TESCEA), kitengo cha huduma za ajira, kinachowaunganisha watafuta kazi na mwajili.
Baadhi ya wanafunzi walioshiriki kongamano hilo.
Picha ya pamoja.
Na Ghisa Abby
CHUO
Kikuu Mzumbe kimeandaa mradi maalumu utakaowawezesha wahitimu kutoka vyuoni
kuweza kujiajiri, kuajirika na kutafuta fursa za kuanzisha biashara.
Makamu
mkuu wa chuo kikuu Mzumbe Profesa Lugano Kusiluka alizungumza hayo wakati wa
kongamano la vijana wanaosoma katika vyuo mbalimbali nchini lililoandaliwa na
chuo hicho ambalo linafahamika kama (TESCEA) kitengo cha huduma za ajira,
kinachowaunganisha watafuta kazi na mwajiri.
Alisema lengo
la kuanzisha mradi huo ni kuzalisha wahitimu wenye elimu, ujuzi na nia kuwawezesha
wahitimu kutoka vyuo mbalimbali kuweza kujiajiri na kupata fursa za kuajiliwa.
Aidha
Profesa Kusiluka alisema kuwa chuo hicho kimetumia wawezeshaji kutoka katika
taasisi za serikali kuweza kuwafundisha vijana waliopo kwenye vyuo vikuu
mbalimbali lengo likiwa kuwaona vijana hao wanapata msaada na kupata fursa
zinazotolewa na serikali ikiwemo mikopo.
Aidha
Kusiluka aliwataka vijana kuacha kutegemea kuajiriwa peke yake bali wawe
wabunifu na kujiajiri.
Kwa
upande wake Mwezeshaji kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Mitengo cha Kazi, Vijana, Ajira
na Watu Wenye Ulemavu, Nassibu Mwaifunga alisema kuwa mfuko wa maendeleo ya
vijana umeanzishwa na serikali lengo likiwa kuwawezesha vijana kuweza kupata
mitaji.
Alisema
kupitia kongamano hilo serikali ina lengo la kuona vijana wengi kutoka vyuo
vikuu wanaweza kutumia fursa zilizopo ili kuweza kujiajiri na kuondoa mawazo ya
kuweza kuajiriwa.
Mkurugenzi
Kitengo cha Huduma za Ajira, Joseph Nganga alisema kuwa kongamano hilo ni
muhimu kwani chuo hicho kimeona namna kuwawezesha vijana kwendana na soko la
ajira.
Pia Serikali
inatekeleza mpango muhimu wa wahitimu kutoka vyuo vikuu vyote nchini kwenda
kufanya kazi kwa muda wa mwaka mmoja kwa mwajili ya kupata ujuzi wa taaluma
aliyonayo kabla ya kuajiriwa.
Aidha,
amewataka vijana wote wanaohitimu kutoka vyuo vikuu kote nchini kutumia fursa
kutoka kitengo huduma za ajira kupata mafunzo yakuweza kuajirika.
Katibu Mtendaji
Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bengi Issa alisema kuwa kama baraza
linasimamia ujasiriamali na kuhakikisha somo lake linafundishwa kwenye vyuo
vyote nchini.
Alisema
pia wanatengeneza mikakati jinsi ya uwezeshaji kwa wananchi kujikomboa hasa
vijana, wanawake kufikia uchumi wa kati.
Baadhi ya
wanafunzi walioudhuria kongamano hilo akiwemo Magdalena wa Mzumbe, alieleza
kuwa wanashukuru uongozi wa chuo kutatua changamoto ya kutembea na bahasha
mkononi kutafuta ajira pindi wanapohitimu masomo yao bali watatumia fursa hiyo
kuweza kuwaelimisha na wenzao.
No comments:
Post a Comment