Wakazi wa jijini Dar es Salaam wakiwa katika viwanja vya
Mbagala Zakhiem kwa ajili ya zoezi la kusajili ili wapate
vyeti vya kuzaliwa.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
WAKALA wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA), umepiga kambi viwanja vya Mbagala Zakhiem kwa ajili ya zoezi la kusajili wananchi ili wapate vyeti vya kuzaliwa.
Zoezi hilo litarahisisha pia wananchi kuwa na taarifa za upatikanaji wa cheti cha kupigia kura cha NIDA.
Kwa mujibu wa Meneja Masoko na Mawasiliano RITA Josephat Kimaro alisema alisema lengo la zoezi hilo ni kusogeza huduma karibu na wananchi na kupanua wigo wa upatikanaji wa huduma za wakala hivyo kuwafikia wananchi wengi zaidi katika maeneo mbalimbali.
Alisema katika siku za hivi karibuni mahitaji ya cheti cha kuzaliwa yameongezeka hasa katika maeneo yote ya nchi ikichangiwa zaidi na wananchi wanaohitaji cheti cha kuzaliwa kwa ajili ya kupata Kitambulisho cha Taifa watakachokitumia kusajili line za simu kwa alama za vidole.
" Kutokana na ongezeko hilo RITA imefanya juhudi mbalimbali kukabiliana na ongezeko la wananchi ikiwa pamoja na kuanzisha vituo vya huduma nje ya ofisi,"alieleza Kimaro.
Alisema kwa zaidi ya miezi miwili RITA imekuwa na kituo katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam ambacho kimekuwa kikisajili wastani wa watu 600 kwa siku.
Alisema kwa zoezi la usajili katika Viwanja vya Zakhiem ni sehemu ya Tamasha la Maisha ni kidole ambalo limeandaliwa na Kituo cha habari cha EFM lililo na.lengo la kutoa elimu kwa wananchi kuhusu usajili kwa njia alama za vidole ambalo pia limeshirikisha wadau wengine kama NIDA, Mamlaka ya Mawasiliani nchini (TCRA) na makampuni yote ya Simu.

No comments:
Post a Comment