Baadhi ya Washiriki wa Mjadala kuhusu Ukuaji wa Miji na Changamoto zake wakifuatilia hotuba ya Naibu Katibu Mkuu
Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Nicolaus Benjamin (Hayupo
pichani) wakati akifungua Mjadala huo jijini Dodoma Leo Tarehe 30 Januari 2020.
Mjadala huo umeandaliwa kwa pamoja na Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya
Makazi na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Makazi (UN Habitat).
Washiriki wakifuatilia uwasilishwaji Mada kwenye Mjadala kuhusu Ukuaji wa Miji
na Changamoto zake uliofanyika jijini Dodoma Leo Tarehe 30 Januari 2020.
Mjadala huo umeandaliwa kwa pamoja na Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya
Makazi na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Makazi (UN Habitat).
Mkurugenzi wa Mipango Miji na Vijiji Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya
Makazi Emaculata Senje akichangia katika Mjadala Kuhusu Ukuaji Miji na
Changamoto zake uliofanyika leo tarehe 30 Januari 2020 jijini Dodoma. Mjadala
huo umeandaliwa kwa pamoja na Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na
Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Makazi (UN Habitat).
Washiriki wa Mjadala kuhusu Ukuaji wa Miji na Changamoto zake
uliofanyika
jijini Dodoma Leo Tarehe 30 Januari 2020 wakiwa katika picha ya pamoja.
Aliyekaa katikati ni Kaimu Mkurugenzi wa Mipango Miji Wizara ya Ardhi
Nyumba na Maendeleo ya Makazi Amulike Mahenge. Mjadala
huo umeandaliwa kwa pamoja na Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya
Makazi na
Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Makazi (UN Habitat). (PICHA ZOTE NA HASSAN MABUYE WIZARA YA
ARDHI).
Na Munir Shemweta, WANMM DODOMA
Imeelezwa kukosekana kwa
sera maalum ya uendelezaji Miji nchini kunachangia kuendelea kuwepo makazi
holela kwenye maeneo mablimbali nchini Tanzania.
Hayo yameelezwa na
Mkurugenzi wa Undelezaji Miji na Vijiji Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dkt Mukuka Hante leo tarehe 30 Januari 2020 wakati wa
Kusanyiko la Mjadala kuhusu Masuala ya Ukuaji Miji na Changamoto zake
lililofanyika jijini Dodoma.
Alisema, kwa sasa nchi
nyingi duniani zina sera maalum ya uendelezaji miji aliyoieleza kuwa inawezesha
kuwepo chombo cha kuleta maendeleo ya miji unaoenda sambamba na huduma za afya, makazi, barabara na huduma nyingine za kijamii.
Hata hivyo, Hante alisema
Serikali iko mbioni kuja na sera ya Uendelezaji Miji aliyoieleza kuwa itakuwa suluhisho
la makazi holela hasa kipindi hiki ambacho miji mingi imeendelea kukuwa kwa
kasi.
Kwa mujibu wa Hante,
Uendelezaji Miji maeneo mbalimbali unatakiwa usiwe kwenye uboreshaji makazi
pekee bali uendane na mjumuiko wa uendelezaji miji na vijiji kwa kuwa maeneo ya
vijiji yanatakiwa pia kuwa na makazi bora yatakayochangia uwekezaji. Aidha, alisema
Miji na Vijiji vinategemeana na iwapo vijiji vitaachwe kujumishwa kwenye mpango
wa uendelezaji miji basi vitaachwa mbali
na wananchi wake kuwa nyuma kimaendeleo.
Mkurugenzi huyo wa
Uendelezaji Miji na Vijiji TAMISEMI alibainisha kuwa, ukuaji miji unatoa fursa ya
uwekezeji kwa wananchi vijijni na kubainisha kuwa pamoja na mkazo kuwekwa
katika uendelezaji miji lakini huduma nyingine kama vile Afya na barabara lazima
ziendelezwe hasa kipindi hiki ambacho Seriali inapoelekea katika uchumi wa kati.
Kwa upande wake Meya wa
Jiji la Dodoma Profesa Davis Mwanfupe alisema ukuaji Miji kwenye maeneo mbalimbali lazima
uendane na upatikanaji huduma muhimu kwa lengo la kukabiliana na changamoto na
fursa zitakazopatikana. Alibainisha kuwa, mjadala unaoendelea kuhusiana na
ukuaji miji unakuja wakati muafaka ambapo dunia iko hatua ya kujadili maendeleo
endelevu kwenye maeneo mbalimbali.
Akifungua Mjadala huo,
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Makazi Nicolaus Benjamin aliwaambia
washiriki wa Mjdala huo kuwa serikali ya Tanzania imekuwa ikifanya jitihada
mbalimbali kuhakikisha inapunguza ama kuondoa makazi holela.
Hata hivyo, aliwataka
washiriki hao kuutumia mjadala huo wa siku moja kutafuta ufumbuzi wa changamoto
za makazi holela sambamba na kuibuka mpango utakaotoa fursa za uwekezaji hasa uendelezaji
miji, uratibu na ushirikiano kati ya wadau katika kufikia lengo.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa
Mipango Miji Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Amulike Mahenge
alisema, kusanyiko la Mjadala kuhusu ukuaji Miji na changamoto zake linafanyika
kwa ushirikiano baina ya Wizara yake na Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia Makazi (UN Habitat) na kuhusisha wadau kutoka mamlaka za upangaji
nchini. Kwa mujibu wa Mahenge, Mjadala huo unaangalia fursa na changamoto
zinazopatikana kutokana na ukuaji Miji na jinsi ya kutumia fursa kuwa na miji
endelevu.
Hata hivyo, Mahenge
alisema kwa sasa idadi ya makazi holela imeanza kupungua nchini kutokana na
jitihada za serikali kuruhusu kampuni binafsi za upangaji na upimaji kushiriki
katika kupanga na kupima maeneo mbalimbali ya nchi.
No comments:
Post a Comment