HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 30, 2020

Prof. Ndalichako ahimiza ufaulu bora Msalato sekondari

 Waziri Profesa Ndalichako akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Msalato iliyopo jijini Dodoma.
 Naibu Katibu Mkuu Tamisemi, Gerald Mweli akizungumza na wanafunzi na walimu wa shule ya sekondari Msalato.
 Mkuu wa Shule ya Sekondari Msalato, Neema Maro, akizungumza alipotembelewa na Waziri Profesa Ndalichako.


Na Mwandishi Wetu

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amefanya ziara ya kukagua ukarabati wa miundombinu ya Shule ya Wasichana ya Sekondari Msalato jijini Dodoma na kuzungumza na wanafunzi.

Baada ya kukagua ukarabati huo Waziri Ndalichako alizungumza na walimu, watumishi na wanafunzi wa shule hiyo na kuwataka kuendeleza juhudi za kuhakikisha shule hiyo inapata  na matokeo mazuri kama ilivyofanya kwa miaka 10 mfululizo ya kuongeza ufaulu na kutopata daraja la sifuri kwenye matokeo ya kidato cha nne.

“Nawapongeza kwa kuwa shule ya wasichana yenye matokeo mazuri kwa kipindi kirefu, niwaombe ongezeni bidii ili matokeo ya elimu bila malipo yaweze kuonekana kwani Rais John Magufuli, anapambana kuhakikisha elimu inakuwa bora ikiwemo kuongeza bajeti ya elimu ya sekondari kwa asilimia 70 mwaka uliopita," alisema Profesa Ndalichako.

Waziri Ndalichako ameeleza kuwa matokeo chanya ya Sera ya Elimu Bila Malipo ni kuongezeka kwa wanafunzi wanaomaliza darasa la saba na kutakiwa kujiunga na kidato cha kwanza huku akijivunia ongezeko la wanafunzi hao kutoka 366,296 mwaka 2016, w 680,000 mwaka 2020, na inatarajiwa Mwaka 2023 watakuwa 1,400,00 na hivyo kuhitajika kuongeza  miundo mbinu ya shule za sekondari kwa zaidi ya asilimia 100.

Alisema katika kuangalia hilo Serikali ilikuja na Mradi wa Kuimarisha Elimu ya Sekondari (SEQUIP) na kuomba ufadhili wa Benki ya Dunia.

Waziri huyo anaamini kwamba Benki ya Dunia itaridhia na kupitisha mradi huo muhimu kwa taifa kwa sababu unakwenda kutatua mahitaji ya haraka ya kielimu kwa watanzania na kutimiza Malengo Endelevu ya Maendeleo.

Waziri Ndalichako amefafanua kuwa kuwa mradi wa ukarabati una lenga kuongeza idadi ya shule za sekondari ambazo zitajengwa karibu na jamii ili watoto wasome katika mazingira salama, kuongeza shule za bweni hususan kwa ajili ya watoto wa kike, upanuzi wa shule kongwe 50 ili kuongeza nafasi na kukamilisha maabara. Kimsingi, wanafunzi zaidi ya 6,000,000 wa kike na kiume watanufaika na Mradi katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Mradi pia utawezesha uboreshaji wa  vituo vya utoaji elimu kwa mfumo mbadala kupitia Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi (FDCs) na Vituo vya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (AEP) Centers na ambao utawezesha wanafunzi awalioacha Shule kwa sababu mbalimbali kupata elimu na kumuwezesha kurejea katika mfumo rasmi.

Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za  Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Elimu, Gerald Mweli alisema ofisi yake  itaendelea kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknlojia  kuhakikisha inakamilisha ukarabati wa shule kongwe kwa kukarabati maeneo ambayo hayakufikiwa katika awamu ya kwanza huku akipongeza juhudi za walimu wa shule hiyo kwa kuondoa daraja sifuri.

Mkuu wa shule ya sekondari Msalato, Neema Maro ameishukuru serikali kwa namna inavyokarabati shule kongwe ikiwa pamoja na kuweka mazingira wezeshi ya ufundishaji na ujifunzaji, huku akiomba kutatuliwa changamoto ya uzio, uchakavu wa baadhi ya miundombinu ambayo bado haijakarabatiwa shuleni hapo.

No comments:

Post a Comment

Pages