Na Irene Mark
MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imetoa taarifa ya hali mbaya ya hewa kwa siku tatu mfululizo kuanzia leo January 27 hadi 29,2020.
Taarifa hiyo ilitolewa Dar es Salaam leo jioni na Meneja wa Utabiri kutoka Kituo Kikuu cha Utabiri, Samuel Mbuya na kusema hali hiyo mbaya ni mvua kubwa hasa kwenye mikoa 12.
Mbuya aliitaja mikoa hiyo kuwa ni Kagera, Mwanza, Geita, Simiyu, Shinyanga, Mara, Tabora, Singida, Dodoma, Manyara, Arusha na Kilimanjaro.
"Mamlaka imetoa angalizo la mvua kubwa kwa baadhi ya maeneo ya mikoa tajwa hivyo wakazi wake wachukue tahadhari za kutosha.
"Watu waache kudharau maji hasa madereva wa vyombo vya moto kuchukua tahadhari sehemu zenye maji mengi," Mbuya.
Pia aliwashauri viongozi wa mitaa kwa kushirikiana na wananchi kusafisha mitaro na kuondoa taka zinazoweza kutuwamisha maji ili kuepuka mafuriko.

No comments:
Post a Comment