Meya wa halmashauri ya Ilala Omary Kumbilamoto akiangalia bidhaa
zinazozalishwa na Taasisi ya Fahari Tuamke Maendeleo (Na Mpiga Picha Wetu).
NA FARAJA EZRA
NA FARAJA EZRA
MEYA
wa Halmashauri ya wilaya ya Ilala Omary Kumbilamoto amewataka Wanawake
wa halmashauri hiyo kujikwamua ili kukuza uchumi wa nchi.
Aidha
Kumbilamoto aliyasema hayo wakati wa kufunga mafunzo ya Wanawake na
Vijana Wajasiriamali wa Kata ya Gongolamboto jini Dar es Salaam
yalioandaliwa na Taasisi ya Fahari Tuamke Maendeleo.
"Nampongeza
Mwenyekiti wa Taasisi ya Fahari Tuamke Maendeleo Neema Mchau, katika
juhudi zake za kuisaidia serikali hasa wilayani Ilala kuwainua wanawake
katika shughuli za uzalishaji kwa kuwapatia ujuzi sasa wanamiliki
viwanda vyao, "alisema Kumbilamboto.
Alisema
imefika sasa Wanawake kusimamia imara katika viwanda vidogovidogo
ambavyo vinazalisha bidhaa na kuzitangaza katika masoko ya ndani na nje.
Hata
hivyo Serikali inaboresha soko la kisasa la Kisutu ambalo ujenzi wake
umegharimu bilioni 13 litakapoanza kutumika soko hilo watawekwa
wafanyabiashara wa awali na nafasi za Wafanyabiashara 700 zitakuwepo.
Hivyo
ameitaka taasisi hiyo na wafanyabiashara kuchangamkia fursa hiyo kwani
soko hilo litakuwa la kisasa na watalii watafikia hapo ndio mradi mkubwa
wa soko la kipekee katika Halmashauri ya Ilala.
Alisema
serikali inatoa mikopo ambayo aina riba kupitia halmashauri kwa vikundi
vinavyotambulika wakopaji wakope fedha hizo na wakumbuke marejesho ili
wengine waweze kukopa .
Naye
Mwenyekiti wa Fahari Tuamke Maendeleo Neema Mchau, amempongeza Meya wa
Ilala Omary Kumbilamoto ambaye ni mlezi wa Taasisi hiyo.
Aidha
Mchau alisema mafunzo hayo yalikuwa ya wiki moja ya utengezaji sabuni,
Mafuta ya kupaka, na sabuni za maji ambapo kila mshiriki amepewa Cheri
cha ushiriki kwa kufanya vizuri ambapo kwa sasa anamiliki Kiwanda
chake.
No comments:
Post a Comment