HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 28, 2020

Vigogo Ngara Farmers wafikishwa Mahakamani, wakosa dhamana


Na Lydia Lugakila, Bukoba

Jeshi la Polisi mkoani Kagera limewafikisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Bukoba watu wanne waliokuwa viongozi wa Chama cha Ushirika Ngara Farmers kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo ubadhilifu wa fedha za wakulima na kukisababishia chama hicho hasara ya zaidi ya Sh. Milioni 14.
 
Wakili wa Serikali, Haruna Shomali, amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Thomson Soyongwe aliyekuwa Mwenyekiti, Paschal Minani aliyekuwa Meneja,  Bazilius Thomas aliyekuwa Mtunza Stoo, Paschal Kangeze, aliyekuwa Mhasibu.


Watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaiwa kukisabishia chama hicho hasara ya zaidi ya Sh. Milioni 14 ambapo makosa hayo yalitendeka kwa nyakati tofauti kwa kipindi cha mwaka 2012 na 2014 wakati wakiwa viongozi wa chama hicho.

Baada ya Hakimu Kapokolo kusikiliza hoja za jamhuri alisema kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo mpaka mahakama ya juu kutokana na mashtaka yanayowakabili ikiwemo la uhujumu uchumi ambalo mashtaka yake yanazidi kiasi cha milioni 10 na haina mamlaka ya kutoa dhamana.

Washtakiwa hao wamerudishwa rumande ambapo kesi hiyo itasikilizwa Februari 11 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

Pages