Mkurugenzi Msaidizi Wizara ya Afya
Idara Kuu Maendeleo ya Jamii, Bw. Sebastian Kitiku, akitoa maelekezo kwa
Wanafunzi wa Sekondari na shule ya Msingi Mtinko iliyoko Wilaya Singida mkoani Singida kuhusu maabukizi ya virusi vya UKIMWI.
Na
Mwandishi Wetu SINGIDA
Viongozi wa Dini
Mkoani Singida wameshitushwa na kiwango cha maambukizi ya UKIMWI hapa Nchini
hasa kwa vijana na kuonya kuwa kama Taifa tusipokuwa makini na malezi kwa
vijana Taifa litazidi kuangamia.
Viongozi hao wadini
kwa nyakati Tofauti Mkoani Singida wamekili kuwepo kwa mmomonyoko wa maadili
kwa vijana unaosababishwa na uzembe wa malezi lakini pia wakitaja uwepo wa uwekezaji
wa kumbi za starehe ambao haujasimamiwa kisheria kuwa unachangia maambukizi
hayo.
Akiongea mapema leo
ofisini kwake Kiongozi wa Kanisa Katoliki Mkoani Singida Askofu Edward Mapunda
amesema watoto wa siku hizi hawana jipya la kujifunza kutoka kwa wazazi wao
kutokana na wazazi hao kujikita zaidi katika kazi za kila siku na kushindwa
kupata nafasi za kulea watoto lakini pia wazazi kushindwa kulinda ndoa zao na
kuishi wakiwa wametengana.
Askofu Mapunda
meongeza kuwa Kanisa linaamini mtu anaweza kuishi bila kufanya ngono kwakuwa
ngono sio ugali, sio juisi, sio pilau wala sio tiba na hakuna aliyewai kufa kwa
kukosa ngono na kuwataka watu kuwa na hofu ya Mungu ili waweze kuepukana na
virusi vya ukimwi.
Aidha Askofu Mapunda
alisema ni lazima kuwaeleza ukweli vijana kwamba wanaweza kuishi bila ngono kwa
kuwa kwa Mungu hakuna msamaha kwani uwezi kumwambia Mungu kuwa umefanya ngono
kwa kuwa haukuwa na sabuni akisisitiza kuwa ni bora ukaoga bila sabuni usipate
ukimwi kuliko kupata ukimwi kwa kuoga na sabuni.
Naye Mkurugenzi
Msaidizi Idara ya Watoto Kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu Maemdeleo ya Jamii Bw.
Sebastian Kitiku akiongea na Vijana wa Shule ya Sekondari Kijota na Mtinko
zilizoko Wilaya Singida alisema kuwa kila mwezi ukipita watu elfu sita wanapata
maabukizi ya virusi vya UKIMWI nchini.
Aidha Bwana Kitiku
aliongeza kuwa ni UKIMWI ni janga la Kitaifa kwani kila Siku ikipita watu 200
wanapata virusi vya ukimwi na kati ya watu hao maambukizi kwa vijana wa miaka
15-24 kwa siku ni 79 na kati ya hao 79 wasichana 63 hupata maabukizi mapya kwa
Siku.
Naye Shekhe wa Mkoa
wa Singida Shekhe Issa Simba akiongea ofisini kwake katika Manispaa ya Singida
pia amesema kuwa kwa mujibu wa Kiongozi wa Dini hiyo Mtume Mohamed anasema kila
ugonjwa una tiba yake lakini ugomjwa wa UKIMWI hauna tiba hivyo kuufananisha na
adhabu na kuwataka watu kutubu na kumurudia Mungu.
Shekhe Issa Simba
amewataka wazazi kumrudia Mungu na kulea watoto wao akionya kuwa tumeacha miiko
ndio maana unakuta mtoto anakuwa wa mwisho kurudi usiku wakati wazazi wapo au
mtoto namiliki simu kubwa kuliko mzazi lakini wazazi wanakaa kimya jambo ambalo
linachangia upungufu wa maadili.
Wakati huo huo Mkuu
wa Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi amesema kuwa Mkoa wa Singida ni
lazima utokomeze maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa kiwango cha asilimia
sifuri akiwataka wadau wote mkoani kwake kuunganisha nguvu ili kutokomeza
maradhi haya.
Aidha Dkt. Nchimbi alisikitishwa na ongezeko la
maambukizi mkoani humo kwani takwimu zinaonesha kuwa maambukizi yameongezeka
kwa kiwango cha asilimia 3.3 mpaka 3.6 jambo ambalo linakwamisha juhudi za Mkoa
katika mapambano dhidi ya ukimwi.
Dkt. Nchimbi ameonya
kuwa ni lazima kukomesha biashara ya ngono ulevi na makumbi ya starehe ambazo
amezitaja kama visababishi vya maambukizi nakuwataka wamiliki wa vyombo hivyo
kufikiria biashara nyingine vilevile akiwataka wafanya biashara ya ngono kuacha
kabisa kwani hakuna mfanya biashara ya aina hiyo aliyewai kuacha urithi wa
maana na wa kuigwa.
Wizara ya Afya Idara
Kuu Maendeleo ya Jamii iko Mkoani Singida kufanya kampeini kwa vijana kuhusu
maambukizi ya ukimwi kampeini amabayo itaendelea kwa Mikoa ya Morogoro na
Dodoma kama mikoa ya mfano na baadae Nchi Nzima kwa kushirikiana na TASAF,
TACAIDS na kufadhiliwa na fedha ya Mfuko wa Dunia(Global Fund).
No comments:
Post a Comment