Mlezi na Mshauri wa Shirika la EMFERD, Josephine Bakita, akizungumza na
waandishi wa habari juu ya Tamasha la kuwaenzi, kuwainua na kuwapandisha
daraja la juu kwa watoto wenye ulemavu na mahitaji maalumu,Tamasha
ambalo litafanyika Desemba 7,2020 Wilayani Mvomero.
Baadhi ya watoto wenye ulemavu na mahitaji maalumu wanaoishi katika
kituo Cha Erick Memorial Foundation for Education and Rehabilitation for
Disabled (EMFERD).Na Ghisa Abby
SHIRIKA
la Erick Memorial Foundation for Education and Rehabilitation For
Disabled (EMFERD) kwa kushirikiana na kanisa Katoliki Parokia ya
Mtakatifu Aloyce Gonzaga Mvomero jimbo katoliki la Morogoro imeandaa
tamasha la kuwaenzi na kuwainua watoto 75 wenye ulemavu na mahitaji
maalumu.
Tamasha hilo linatarajiwa kufanyika Februari 7,2020 wilayani Mvomero mkoani Morogoro.
Mlezi
na Mshauri wa Shirika la EMFERD Josephine Bakita ameeleza hayo leo
Januari 27,2020a wakati akizungumza na waandishi wa habari Morogoro.
Mlezi
huyo amesema tamasha hilo limedhaminiwa na taasisi ya kimarekani
ijulikanayo Tim Tebow, na limelenga kuufanya usiku wa Mwangaza maarufu
kama 'NIGHT TO SHINE, kwa watoto wanaoishi na ulemavu wa aina
mbalimbali.
Bakita
amesema lengo la tamasha hilo ni kuikumbusha jamii sambamba na
kuyakumbusha makanisha na madhehebu ya dini kwa ujumla kuwasogeza karibu
watoto wenye mahitaji maalumu kwa kuwapa ukaribisho maalumu katika viti
vya enzi.
Amesema hiyo
inafanyika kwa kuwa imeonekana katika baadhi ya makanisa na madhehebu
mbalimbali watu wenye ulemevu hususani watoto wamekuwa hawapewi
kipaumbele na nafasi sawa na watu wengine.
Historia
ya tamasha hilo ilianzishwa na mchezaji mpira maarufu wa nchini
MarekaniTim Tebow na limekuwa likifanyika kila Febrauri 7 kila mwaka
katika nchi mbalimbali duniani na kulenga kuwapa heshima na hadhi ya
juu watu wenye mahitaji hasa watoto ambapo kwa Tanzania tamasha hilo ni
la kwanza kufanyika.
“Hili
Tamasha lina mguso sana kwa watu wenye mahitaji maalumu, hivyo tunaomba
wadau wengine nchini kuwezesha na kushirikiana na EMFERD kuwezesha ili
kufanikisha,” amesema
Kwa
upande wake Afisa Habari wa Shirika la EMFERD, Victor Makinda amesema
watoto 75 wenye mahitaji maalumu watashirikia natika tamasha hilo huku
wakiwa na familia zao kwa ajili ya uangalizi.
“Kubwa
zaidi lililolengwa ni kuwainua watoto kuwapa daraja la juu zaidi kwa
kuhakikisha tunalula nao, na kuheshimiwa huku tukiwapa nafasi ambayo
pengine kwenye jamii zao hanaikosa,”amesema.
Aidha
Tamasha hilo linatarajiwa kufanyika Februari 7,2020 wilayani Mvomero
mkoani Morogoro na Taasisi ya EMFERD imekuwa ikiwalea watoto wenye
ulemavu wa akili na viungo.
No comments:
Post a Comment