NA
TIGANYA VINCENT
HALMASHAURI ya Manispaa ya Tabora imefanikiwa kutoa mikopo ya jumla
ya shilingi milioni 190 kwa vikundi 36.
Fedha hizo zimetolewa hadi kufikia Desemba mwaka jana ikiwa ni
sehemu ya mikopo ya asilimia 10 inayotokana na mapato yake ya ndani.
Taarifa hiyo imetolewa leo na Mchumi wa Manispaa ya Tabora
Joseph Kashushura wakati kikao cha Maalumu wa kupitia makisio ya mapato na
matumizi ya Bajeti wa Baraza la Madiwani ya Manispa.
Alisema kati ya fedha hizo shilingi milioni 115 zimetolewa kwa
vikundi 23 vya wakina mama , milioni 55 zimetolewa kwa vikundi 9 vya vijana na
milioni 20 zimetolewa kwa vikundi vinne(4) vya walemavu.
Katika hatua nyingine
Kashushura alisema kuwa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora imefanikiwa
kupeleka kiasi cha milioni 119.4 katika Kata 19 ili kutekeleza miradi ya
maendeleo.
Wakati huo huo Kashushula amesema kuwa Halmashauri hiyo imepokea
Jumla ya shilingi milioni 899.2 ambazo zimetumika katika ukarabati wa
miundombinu ya Shule ya Sekondari ya Kazima.
Alizitaja kazi zilizofanyika ni ukarabati wa vyumba 6
vilivyokuwa vimeungua , ukarabati wa bweni la wasichana na bweni la wavulana, ukarabati
wa vyumba 6 vya block Na .1 na ukarabati vya vyoo vya walimu na wanafunzi.
Kashushura aliongeza kazi nyingine ni ukarabati wa mfumo wa maji
taka, ukarabati wa darasa la walemavu,
ukarabati wa vyumba vya block 23, ukarabati wa maabara ya kemia, bailojia, ,
fizikia, ukarabati wa karakana ili liwe bweni la wasichana.
Aliongeza kuwa Manispaa ya Tabora imepokea jumla ya milioni 522
kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu ya Shule ya Sekondari Milambo.
Kashushura alisema ukarabati huo umehusisha ukarabati wa madarasa,
jengo la utawala, vyoo, maabara na jengo la chakula.
No comments:
Post a Comment