Na Lydia Lugakila, Kagera
SHIRIKA la Kwa Wazee
Nshamba lililoko wilayani Muleba mkoani Kagera wametekeleza agizo la Katibu Mkuu
wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Dk.
Bashiru Ally la kuhakikisha wanaunda mabaraza ya wazee ya chama hicho yatakayosaidia
kuwaunganisha ili waweze kutambuliwa na kupata huduma za muhimu na stahiki zao
ikiwemo pensheni.
DK. Bashiru alitoa
agizo hilo Januari mosi mwaka huu baada ya kukutana na kufanya mazumgumzo na
shirika hilo alipokuwa likizo nyumbani kwake Kanazi Bukoba vijijini ambapo katika mazungumzo hayo, pamoja na
mambo mengine, shirika hilo linayojumuisha wazee 29, 945 kutoka kila Kata,
Wilayani Muleba pia waliipongeza CCM kwa kuanzisha utaratibu wa Mabaraza ya
Wazee katika kila ngazi na wao wakaahidi kuwa mstari wa mbele kuhamasisha wazee
wote wanajiunga kwenye mabaraza hayo ili changamoto zao zipate urahisi wa
kusikilizwa na kutatuliwa kwa pamoja.
Akizungumza, Mkurugenzi
wa shirika hilo Lydia Lugazia kwa niaba ya wazee wa taasisi hiyo alisema baada ya kuasisiwa taratibu hizo, wamefarijika
kwa kuwa sasa watapata sehemu sahihi ya kupeleka changamoto zao kwa pamoja na
kwa kuwa wao walianzisha mabaraza huru yanayowaweka pamoja chini ya Taaisi ya
KWA WAZEE, hivyo wakaahidi kutoa ushirikiano na kuhamasisha wazee wote wawe
kwenye Mabaraza hayo ili changamoto zao zitatuliwe kwa pamoja.
"Mwanzoni mwa mwaka
huu tuliombwa na Dk. Bashiru kwamba shirika letu tushirikiane na Halmashauri ya
Wilaya ya Muleba kuunda mabaraza ya wazee ili kupata huduma mbalimbali tukiwa
kwenye chombo kinachotambulika kitaifa hivyo sisi bila kusubiri tumetekeleza
agizo hilo"alieleza Lydia.
Katika mazungumzo hayo
yaliyofanyika Januari mosi mwaka huu, Dk. Bashiru aliwahakikishia nia ya dhati
ya Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Pombe
Magufuli ya kuunda mabaraza hayo ni kuwa karibu zaidi na wazee na siku zote
amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha changomoto zao mbalimbali zikiwemo za Afya
zinatatuliwa hivyo akawataka kuhakikisha wanasimamia na kukamilisha mabaraza
hayo mapema ili wazee waweze kutambuliwa na kupata haki na stahiki zao kwani
wao ni hazina kubwa ya Taifa hili.
Elena Bejumla (65) alisema
wao wanaofadhiriwa na shirika hilo wameweza kupatiwa pensheni ya kila mwezi
kiasi cha shilingi 14,500 kwa kila mmoja pia wanapewa huduma ya utetezi wa
kisheria pale wanapofanyiwa vitendo vya unyanyasaji, udhalilishaji na
kuwasaidia kupata matibabu, kuwasaidia kulea yatima walioachiwa na watoto wao.
"Ninaimani
tukiunda mabaraza ya CCM, huduma hii itawafikia wazee wengi maana kuachia
shirika peke yake halitoweza kutumudu sote kwa sababu kila siku wazee
wanaongezaka na pia wapo ambao bado shirika halijawafikia watapata msaada sasa
chini ya CCM, "alileza Elena.
Willard Byamungu (70)
alisema wanaishukuru CCM kwa juhudi inazofanya za kuhakikisha wazee
wanatambuliwa ili kuwezesha kupata huduma zinazostahili.
"Agizo la Dk. Bashiru
limetekelezeka maana ndani ya wiki moja tangu ameondoka tumepigwa picha na
shirika la kwa wazee, tumepewa vitambulisho ambapo tumeambiwa vitatusaidia
kupata huduma bora za matibabu, utaratibu wa kulipwa pensheni, kuthaminiwa hata
pale tunapoenda kupiga kura tulikuwa tunasubiri huko nyuma muda unaisha
tunaondoka lakini sasa nikivaa kitambulisho changu shingoni watanipa kipaumbele,"alisema
Byamungu.
Kwa upande wa Katibu wa Jumuiya ya Wazazi wa
CCM, Wilaya ya Muleba Kengela Magesa alisema
baada ya kukamilisha zoezi la kupigwa
picha na kuunda mabaraza 43 yenye wanachama 29,945 katika mkutano wa adhara
uliofanyika Kata ya Biilabo ambapo, aliwaelezea wazee kuwa agizo la Katibu mkuu
linaendea kutekelezwa nchi nzima kwani Taifa linajipanga namna ya kuwaenzi
wazee kwani wameshiriki kufanya mambo mengi katika kuikomboa nchi yetu ikiwemo vita
vya Kagera.
"Nashukuru
shirika hili uongozi wao walichukua
jukumu la kumuona na kumuelezea katibu mkuu dhamira yao ndipo akaeleza kuwa
mambo haya yashuke kuanzia ngazi ya chini ndipo hawa wakapewa jukumu hili la
kuunda mabaraza ya CCM ili muweze kupaza sauti kwa pamoja hivyo wametekeleza"alisema Magesa.
Katibu wa Jumuhiya ya Wazazi CCM wilayani Muleba akizungumza na wazee.
Baadhi ya wazee hao wakitoa pongezi kwa shirika hilo pamoja na serikali.
Mkurugenzi wa Shirika la Kwa Wazee Nshamba wilayani Muleba Lydia Lugazia akizungumza na wazee.
No comments:
Post a Comment