NA TIGANYA VINCENT, TABORA
KAMPUNI
ya Tumbaku ya Alliance One Tanzania (AOTTL) imeukabidhi uongozi wa
Mkoa wa Tabora vifaa mbalimbali vikiwemo vifaa tibaa na
ujenzi vyenye thamani ya shilingi milioni 19.8.
Msaada huo umekabidhiwa
leo na Mkurugenzi wa Uzalishaji wa Kampuni hiyo David Mayunga kwa Mkuu wa Mkoa
wa Tabora Aggrey Mwanri katika halfa iliyofanyika Ofisini kwake.
Mayunga alivitaja vifaa
vilivyotolewa ni Bati 200, Saruji mifuko 250, magodoro 30, shuka za wagonjwa
110, vitanda vya wagonjwa 3 na kitanda maalumu kwa ajili ya mama kujifungulia
kimoja.
Alisema msaada huo
utapelekwa katika Kituo cha Afya cha Mazinge na Kituo cha Afya cha Mwamayunga
vilivyopo wilayani sikonge na Zahanati ya Igagala wilayani Kaliua.
Mayunga alisema Kampuni
hiyo imeamua kutoa msaada huo kupitia mpango wa ujerejeshaji wa huduma kwa ili
kuunga mkoano juhudi za Serikali za kuboresha huduma za afya na kuwapunguzia
adha wananchi wa kwenda kupata huduma hizo mbali.
Naye Mkuu wa Mkoa wa
Tabora Mwanri aliitaka Idara ya Afya ya Mkoa huo kuhakikisha vifaa hivyo vinatunzwa
na kutumika kwa malengo ya utoaji wa huduma bora kwa wananchi.
Alionya kuwa
hatasitakuchua hatua kwa watendaji wote waliopewa dhamana ya kutunza vifaa
kuhakikisha haviibiwi na kupelekwa kwenye majumba ya watu au kwa watoa huduma
ya afya ambao sio walengwa.
Kwa upande wa Mkuu wa
Wilaya ya Kaliua Abel Busalama aliishukuru Kampuni ya Alliance One kwa msaada
ya vitanda walivyotoa kwa ajili ya kuongezea nguvu Zahanati ya Igagala.
Alisema hatua hiyo ni
muhimu katika kukabiliana na msongamano wa kupata vifaa vya kulaza wagonjwa
katika Zahanati hiyo.
Busalama alisema kutokana
na Zahanati hiyo kupata wagonjwa wengi kutoka sehemu mbalimbali wanao mpango wa
kujenga Kituo cha afya katika eneo hilo kwa kushirikiana na Halmashauri ya
Wilaya ya Kaliua , nguvu za wananchi na kuomba wadau wengine kuunga mkono
juhudi hizo.
No comments:
Post a Comment