NAIBU
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha, ameitaka
Taasisi za mafunzo na wadau wa sekta ya Utalii kufanya kazi kwa weledi
pamoja ili kutatua changamto zilizopo ili kufikia uchumi wa kati ifikapo
mwaka 2020.
Akizungumza
na wadau hao jana jijini Dar es Salaam wakati wa kufunga Kongamano la
Kimataifa la kuunganisha wanataaluma na wadau wa sekta ya Utalii na
Ukarimu jijini humo.
Aidha
alisema kumekuwepo na ushindani mkubwa katika soko hivi sasa kutokana
na kuongezeka kwa wataalamu hao hivyo kunahitajika maandalizi mazuri ya
rasilimali watu ili kuweza kushindana katika soko la dunia.
Waziri
Ole Nasha alisema ya sekta ya Utalii ni moja ya Sekta inayolipatia
Taifa fedha za kigeni kutokana na utalii hivyo alisema kukiwa na nguvu
kazi yenye weledi na ufanisi wa kutosha nchi itaneemeka kupitia utalii.
“Hakika
tunahitaji kuandaa vizuri rasilimali watu, nchi jirani zimepiga hatua
kwenye kuvutia watalii sio kwamba wana vivutio vingi kuliko sisi ni
kutokana na pamoja na mambo mengine kuwa na nguvu kazi yenye weledi ndio
maana kama Taifa tunawekeza katika kutayarisha vijana ili kuwa na nguvu
kazi yenye weledi katika sekta ya utalii,” alisema na kuongeza.
"Taifa
letu linatoa kipaumbele katika kuimarisha viwanda ili kuleta mabadiliko
ya kiuchumi ikiwa ni pamoja na kuandaa nguvu kazi, hivyo ni vizuri
kukawa na mfumo wa mafunzo pacha kati ya Taasisi za mafunzo na wamiliki
wa viwanda", alisema Ole Nasha.
Hata
hivyo ameipongeza chuo cha Taifa cha Utalii na Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam kwa kuandaa mkutano wa kuwaunganisha wakufunzi na watoe huduma
hiyo walio katika biashara ya Utalii kwani kwa pamoja wanaweza kutatua
changamoto zilizopo.
Naye
Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii, Dkt. Shogo Mlozi amewataka
kuendeleza ushirikiano na vyuo vingine vinavyotoa mafunzo ya utalii ili
kuimarisha mpango wa utoaji mafunzo kwa kufanya kazi na watoa huduma
ili kupata nguvu kazi yenye weledi na ujuzi kwa maslahi ya Taifa.
Alisema
Soko la hotelia hivi sasa linapaswa kutoa nafasi kwa ajili ya walimu
kupata ujuzi kwani kwa kufanya hivyo nchi itakuwa ya kwanza kuongoza
kwenye sekta ya utalii na ukarimu nchini.
Pia
Mlozi amesisitiza kuendeleza ushirikiano kati ya Taasisi hizo na
wamiliki wa viwanda ili kuweza kutatua changamoto za ajira kwa vijana.
No comments:
Post a Comment