HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 21, 2020

TAMASHA LA KUMBUKIZI YA MIAKA 113 YA VITA VYA MAJIMAJI KUANZA FEBRUARI 22, 2020

Na Asha Mwakyonde

WIZARA  ya Maliasili na Utalii kupitia Taasisi ya Makumbusho ya Taifa imeeandaa tamasha la Kumbukizi la miaka 113 la Vita vya  Maji Maji  lengo kuu likiwa ni kuwakumbuka mashujaa waliopigana na waliokufa Waite teya  maslahi mapana ya nchi.

Tamasha hilo  Februari 22 hadi 27 mwaka huu mjini Songea huku kaulimbiu ikiwa ni " Mchango wa vita vya Maji Maji katika kuendeleza na kurithisha Urithi wa Utamaduni  kwa maendeleo ya Taifa.

Akizungumza  jijini Dar es Salaam Februari 18, mwaka huu Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa, Dk. Noel Lwoga amesema  Februari 27, mwaka 1906 mashujaa wa vita 67, walinyongwa na Wajerumani mjini Songea na kuzikwa katika makaburi mawili yaliyopo Makumbusho ya Maji Maji.

Mkurugenzi huyo amesema kuwa malengo mengine ya maadhimisho hayo ni kutoa fursa  kwa wananchi hususani wa Mkoa wa Ruvuma kuenzi ,kutunza  na kuendeleza urithi asili pamoja na utamaduni kwa ajili ya kizazi cha sasa na kijacho.

Dk. Lwoga  amefafanua kuwa lengo jingine ni kuibua na kuendeleza fursa za utalii wa utanaduni wa Mkoa wa Ruvuma na ukanda wa kusini  ili kuinua uchumi na iuboresha hali ya maisha ya wananchi wa eneo hilo.

Amesrma kuwa maadhimisho hayo yataambatana na shughuli mbalimbali kama kutoa elimu shuleni, maeneo ya wazi pamoja na maonesho ya wazi ya wajasiliamali.

“Urithi huu ni tunu na kioo cha taifa la Tanzania, na utaleta umoja, Amani na utangamano  wa kitaifa, ikiwa ni pamoja na kulitambulisha taifa la Tanzania katika dunia ya sasa,”amesema Dk. Lwoga.
.
Naye  Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya maadhimisho hayo, Christine Ngereza amesema watatoa elimu kwa shule 16 za mkoa huo ili kuhamasisha mila na utamaduni pamoja na kuzihifadhi.

“Tutatoa elimu ya kuhamasisha jamii kuanzisha makumbusho  na kuyafanya kuwa ya kiutalii.Tutatembelea eneo la chifu msaidizi alikuwa akijificha," amesema.

Maadhimisho hayo Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma anatarajia kuwa mgeni rasmi ambapo machifu kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini watahudhuria ikiwa nchi za Malawi na Zambia.

Kumbukizi hiyo  imeandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Taasisi ya Makumbusho ya Taifa imeshirikiana na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Baraza la Mila na Desituri la  Mkoa huo, Jeshi la Wananchi wa Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Pages