Mtaalam wa Huduma za Kidigitali za Tigo, Ikunda Ngowi, akizungumza wakati akitangaza promosheni maalumu ijulikanayo kama‘Toa
bei na Ushinde’ au Bid-2-Win kwa ajili ya wateja wa kampuni hiyo.
Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Simu ya Tigo Tanzania imekuja na promosheni ijulikanayo kama‘Toa
bei na Ushinde’ au Bid-2-Win.
Akitangaza promosheni hiyo jijini Dar es
Salaam Mtaalam wa Huduma za Kidigitali za Tigo, Ikunda Ngowi alisema promosheni
hiyo ni maalumu kwa ajili ya wateja wa Tigo ikiwa ni sehemu ya kuonesha
shukrani zao kwa kuendelea kuwaamini na kutumia mtandao huo.
“Promosheni hii inatoa nafasi kwa wateja
kununua bidhaa mbalimbali kwa bei ya chini au pungufu.Katika promosheni hii
wateja wateweza kujishindia zawadi zenye thamani ya hadi shilingi milioni 5.
Kimsingi,
‘Toa bei Ushinde’ ni huduma ambayo inampa nafasi mteja kushinda bidhaa
aipendayo kila wiki kila anaposhiriki kwa kutaja bei ambayo anaweza kununua
bidhaa hiyo,” alisema.
Mtaalam huyo alisema zawadi hizo
zinahusisha bidhaa za kisasa na za kibunifu zikiwemo simu janja aina ya
Samsung A30, A70, A50, Home internet routers pamoja na Playstations aina ya
Sony ambapo bei ya chini ya kuanzia ni shilingi 1000.
“Tunafurahi kuzindua rasmi promosheni
hii na tunaamini kuwa itawapa nafasi wateja wa Tigo kupata bidhaa za kidigitali
kwa gharama nafuu, huduma hii ni ya haki na inampa kila mteja nafasi ya
kushinda zawadi mbalimbali kulingana na thamani yake,” aliongeza.
Alisema kama kampuni ya kidigitali, wanatambua
mahitaji ya wateja wao ndio maana siku zote wapo mstari wa mbele kuleta
suluhisho zenye kuboresha namna watu wanavyotumia huduma za mawasiliano.
Ngowi alisema huduma hii inamruhusu
mteja kutoa bei ya bidhaa husika na kumpa nafasi ya kushinda bidhaa hiyo. “Tunaamini
kupitia promosheni hii tutafungua njia kwa Watanzania wengi kutumia teknolojia
za kidigitali,” alisema.
Alisema
ni imani yao kuwa, huduma hiyo itapungumza makali ya bei za bidhaa na kuwapa
nafasi wateja kumiliki bidhaa wazipendazo kwa gharama nafuu kwa urahisi zaidi
kupitia Tigo.
Alisema Tigo imekuwa mstari wa mbele
kuleta mapinduzi ya kidigitali ikiwamo kuanzisha huduma ya
Simu janja (Smartphone) ya Kiswahili,
Facebook ya bure, App ya Tigo Pesa na zaidi kuwa kampuni ya Kwanza kutoa huduma
ya kutuma na kupokea pesa katika nchi za Afrika Mashariki.
“Ni imani yetu kuwa, Huduma hii pia
itapungumza makali ya bei za bidhaa na kuwapa nafasi wateja kumiliki bidhaa
wazipendazo kwa gharama nafuu kwa urahisi zaidi kupitia Tigo.
Hivyo basi, tunawahimiza wateja wetu
kushiriki kwa wingi katika promosheni hiyo kwani kadiri unavyoshiriki ndivyo
unavyojiweka katika nafasi nzuri zaidi ya kushinda.
Ili kushiriki mteja wa Tigo anaweza
kutuma ujumbe mfupi meseji wenye neno BID kwenda 15371.Kila meseji itatozwa
kiasi cha shilingi 50 na washindi watapatikana kila wiki,” alisema.
No comments:
Post a Comment