Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) imeunda Kamati ya Maendeleo ya Miradi ili kusimamia
utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa vituo vya michezo vya Kigamboni, Dar
es Salaam na Tanga.
Kabla
ya kuunda Kamati hiyo, Kamati ya Utendaji ilipokea taarifa ya
maandalizi ya utekelezaji wa miradi hiyo kwenye kikao chake
kilichofanyika Februari 18, 2020 jijini Dar es Salaam.
Wajumbe wa Kamati hiyo ni QS Lucy Mzengi (Mwenyekiti), Mhandisi Hersi Said, Mhandisi Hamad Ramadhan, na Mhandisi Charles Adrian.
Kikao
hicho cha kawaida vilevile kilipokea Taarifa ya Rais, Taarifa ya
Utekelezaji ya Sekretarieti, Utekelezaji wa Mpango Mkakati wa TFF
(StrategicPlan) kwa mwaka 2020 na kufanya uteuzi wa Kamati ndogo za TFF.
Wajumbe
walioteuliwa katika Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ni
Mwanasheria Elias Mwanjala (Mwenyekiti), Said Soud (Makamu Mwenyekiti),
Zakaria Hans Poppe, Issa Batenga, Wakili Msanifu Kondo, na Said George.
Kamati
ya Fedha na Mipango ni Athumani Nyamlani (Mwenyekiti), Francis Ndulane
(Makamu Mwenyekiti), Pascal Kihanga, Maxmillian Tabonwa, Paul Bilabaye,
Allen Mrindoko, Evans Mgeusa, na Seif Muba.
Kamati
ya Mashindano ni Ahmed Mgoyi (Mwenyekiti), Saloum Chama (Makamu
Mwenyekiti), James Mhagama, Patrick Kahemele, Fortunatus Kalewa, Shafih
Dauda, Sarah Chao, Said Tully, na Ali Kamwe.
Kamati
ya Ufundi ni Vedastus Lufano (Mwenyekiti), Mrisho Bukuku (Makamu
Mwenyekiti), Ibrahim Masoud, Ally Mayay, Michael Bundala, Jumbe Menye,na
Edibily Lunyamila.
Kamati
ya Mpira wa Vijana ni Khalid Abdallah (Mwenyekiti), Lameck Nyambaya
(Makamu Mwenyekiti), Mohamed Aden, Nassib Mabrouk, Salim Kibwana, Vicent
Majili, Kenneth Pesambili, Nicky Magarinza, na Philip Alando.
Kamati ya Waamuzi ni Soud Abdi (Mwenyekiti), Israel Nkongo (Makamu Mwenyekiti), Zahra Mohamed, John Kanyenye, na Samwel Mpenzu.
Kamati
ya Mpira wa Wanawake ni Amina Karuma (Mwenyekiti), Mia Mjengwa (Makamu
Mwenyekiti), Rose Kisiwa, Somoe Ng’itu, Zena Chande, Beatrice Mgaya,
Sofia Tigalyoma, na Zabibu Juma.
Kamati
ya Habari na Masoko ni Steven Mnguto (Mwenyekiti), Osuri Kosuri(Makamu
Mwenyekiti),Cyprian Kuyava, Mgaya Kingoba, Dk. Omar Saleh, na Saleh
Ally.
Kamati ya Tiba ni
Dk. Paul Marealle (Mwenyekiti), Dk. Fred Limbanga (Makamu Mwenyekiti),
Dk. Norman Sabuni, Dk. Lisobina Kisongo, Dk. Eliezer Ndama, Dk. Billy
Haonga, na Dk. Violet Lupondo.
Kamati ya Futsal na Beach Soccer ni Blassy Kiondo, Isaac Munisi, na Didas Zimbihile.
Kamati
ya Leseni za Klabu ni Wakili Lloyd Nchunga (Mwenyekiti), Wakili
Emmanuel Matondo (Makamu Mwenyekiti), Sunday Kayuni, George Mayawa, na
Tumaini Mringo.
Kamati
ya Rufani za Leseni ni Dk. Damas Ndumbaro (Mwenyekiti), Dk. Alex
Mgongolwa (Makamu Mwenyekiti), Charles Matoke, David Kivembele, na
Robert Selasela.
No comments:
Post a Comment