HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 07, 2020

UVCCM YAWAFARIJI WAGONJWA KAGERA

UVCCM Kagera wakiwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa kuazimisha miaka 43 kuzaliwa CCM.


Na Alodia Dominick, Bukoba

Kaimu Katibu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera, Deodatha Mgisha, ameishukuru serikali kwa kuendelea kupanua hospitali hiyo na kuongeza huduma mbalimbali.

Kaimu Katibu huyo ameyasema hayo leo wakati vijana wa chama cha mapinduzi mkoa wa Kagera katika kuadhimisha miaka 43 ya kuzaliwa  kwa chama hicho wametembelea hospitali hiyo na kupanda miti pamoja na kugawa vitu mbalimbali kwa wagonjwa.

Mgisha amesema, katika kutekeleza ilani ya chama tawala miradi mbalimbali imetekelezwa ikiwemo vyumba viwili vya upasuaji kwa akina mama pamoja na chumba cha kujifungulia kwa akina mama ambapo awali akina mama walikuwa wanafanyiwa upasuaji kwenye chumba kimoja na watu wengine ambapo vyumba vikikamilika watakuwa wanafanyiwa upasuaji katika vyumba vyao pekee na awali chumba cha kujifungulia kilikuwa na vitanda 4 na kinachojengwa kikikamilika kitakuwa kinabeba vitanda 10.

Mafanikio mengine aliyoyataja ni pamoja na madactari bingwa wanane wamepelekwa masomoni na serikali, watumishi 26 wameajiliwa hospitalini hapo na 56 wamepandishwa vyeo, imenunuliwa exray digital, gari la kubeba wagonjwa na mashine ya kusafisha figo.

Kwa upande wake katibu mwenezi wa ccm mkoa wa Kagera Amimu Muhamudu ameuahidi uongozi wa hosipitali hiyo kuendeleza ushirikiano kati ya chama na hospitali na akauomba msamaha uongozi wa hospitali hiyo endapo kuna mambo hayakwenda sawa.

Naye Katibu UVCCM Mkoa wa Kagera, Salumu Suleimani, ametaja vitu vilivyopelekwa hospitalini hapo kuwa ni pamoja na upandaji wa miti 150 ikiwemo ya matunda mbalimbali kama maparachichi, machungwa mapera maembe ipatayo 50 na miti ya mbao 100.

Amesema katika wodi ya akina mama na watoto wamegawa sabuni za kufulia na kuogea, biskuti maji na juisi vyenye thamani ya shilingi laki nne.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dkt. Museleta Nyakiroto, ametaja kuwepo changamoto ya daktari wa wazee katika hospitali hiyo richa ya kuwepo kwa dirisha la wazee na kuwa bado swala la uchangiaji wa huduma ya hospitali kwa wazee haijaeleweka sana ingawa kwenye jamii wanajua wazee wanatibiwa bure hivyo kuna mkanganyiko katika vitambulisho vinavyotolewa na halmashauri pamoja na msamaha wa kutibiwa bure.

No comments:

Post a Comment

Pages