HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 24, 2020

WAHADHIRI TUDARCo WAWAFUNDA WANAFUNZI


Na Mwandishi Wetu

WAHADHIRI wa Chuo Kikuu cha Tumàini Kampasi ya Dar es Salaam wamewataka wanafunzi wanaochukua somo la Mahusiano ya Umma (PR) pindi watakapohitimu masomo yao kujitolea na kushirikiana na jamii popote waendapo.

Walitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki wakati wanafunzi wanaochukua somo hilo wakitekeleza kwa vitendo kwa kujumuika pamoja na wafanyakazi, watoa huduma za usafi na chakula wakati wa kufanya kwa vitendo Jukumu la Taasisi Kijamii (CRS) iliyofanyika chuoni hapo.

 Wanafunzi hao wa PR walijumuika pamoja nà jamii ya watoa huduma chuoni kwa kucheza michezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kukimbia,kucheza muziki,kuimba ba michezo mingine.

Mhadhili wa somo la PR, Mary Kafyome, alisema amekua wakifundisha somo hilo kwa vitendo ili kuwajengà wanafunzi hao kuwaza kujitolea kwa vitendo katika jamii pia.

Amesema toka mwaka 2017 akiwa na wanafunzi wanaochukua PR amèpwapeleka wanafunzi hao Sinza hospital kuona wagonjwa kufanya usafi na kutoa zawadi mbalimbali kwa wagonjwa.

Pia amesema aliwahi kufanya ziara ya kùwatembelea wasichana waliokuwa wapishi katika mazingira magumu wanaolelewa eneo la Kimara na kushiriki nao usafiwa maziñgira katika kituo hiko.

"Lakini kwa mwaka huu nimeona tufanye shughuli hizo ndani kwa kujumuika pamoja na wafanyakazi wa usafi na watoe huduma ya chakula kwa wanafunzi na walimu lengo kuongoza mahusiano mazuri pia,"

"Na lengo la kufanya hivi ni kwamba watakapomaliza chuo huko watakapoenda wazingatie makundi mbalimbali ya kijamii ,"àliongeza Kafyome.

Naye Mkurugenzi wa Global Publisher ambaye pia ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu PR chuoni hapo alisema katika maisha kuna mambo matatu ya kuzingatia ikiwemo nidhamu,kujituma na kutokata tamaa .

Hivyo aaliwatakawanafunzi watakapohitimu kuzingatia hayo ikiwa ni pamoja na kufanya kazi kwa bidii bila kujali hali yake ya kuwa na mlango mdogo wa kujipatia kipato.

Naye Mkuu wa Kitengo cha BMC, Ajuae Mdegela naye alisisitiza nidhamu na kùjituma pia pindi watakapokuwa wamemaliza chuo sambamba na kuwa wàbunifu wa kutumia taaluma yao kujipatia kipato.

Naye mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa PR, Mgaya Kingoba, alisema kitengo hiko kilichofanyika chuoni hapo ni kizuri kwani kinajenga upendo baina ya jamii.

No comments:

Post a Comment

Pages