HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 22, 2025

UPINZANI KUKOSA MWELEKEO: CCM YATUPIA LAWAMA SERA DHAIFU

Na Mbaruku Yusuph, Handeni 


KUTOKUAMINIKA kwa sera za vyama vya upinzani kumepelekea kuporomoka kwa mvuto wao kisiasa na hatimaye kushindwa kushindana kwa ufanisi katika ulingo wa siasa nchini.

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga, Rajab Abdurahman, wakati akihutubia wananchi wa Kata ya Chanika, Wilaya ya Handeni, katika ziara ya kampeni kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025.
Rajab, ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC), alisema kuwa CCM ndicho chama pekee kinachotoa ahadi kwa wananchi na kuzitekeleza, tofauti na vyama vya upinzani ambavyo hujitokeza tu wakati wa uchaguzi.

“Vyama hivi vya upinzani huonekana nyakati za uchaguzi tu, lakini baada ya hapo havina uendelevu wala mwelekeo wa kweli wa kuwahudumia wananchi,” alisema Rajab.

Aidha, alisisitiza kuwa kwa kutambua umuhimu wa mfumo wa vyama vingi kwa maendeleo ya taifa, CCM ilifanya uamuzi mgumu kuruhusu uwepo wa vyama hivyo kwa maslahi mapana ya taifa.

“Hawa ndugu zangu wa upinzani wanapaswa kutambua kuwa bila CCM, mfumo wa vyama vingi usingekuwepo,” aliongeza.

Rajab pia alieleza kuwa mbali na jukumu la kudumisha amani, CCM imeendelea kusimamia kwa mafanikio sekta muhimu kama elimu, afya na huduma nyingine za kijamii, akisema kuwa hayo ni mafanikio ambayo vyama vya upinzani haviwezi kuyatekeleza kwa kiwango hicho.

Alimalizia kwa kuwataka wananchi wa Handeni na taifa kwa ujumla kuwachagua wagombea kutoka CCM, akisisitiza kuwa hao ndio viongozi wazalendo wenye nia ya dhati ya kulitumikia taifa.

Kwa upande wake mgombea Ubunge wa Handeni Mjini kupitia Chama cha Mapinduzi Gwakila Reuben alisema anajua maji ndio kilio kikubwa cha wananchi wa Handeni na kuongeza kuwa CCM ndio Chama pekee kianchoweza kumaliza tatizo hilo. 

Gwakila alisema tatizo la maji litamalizwa na Chama cha Mapinduzi chama ambacho ahadi zake ndio zinazotekelezeka tofauti na vyama vya upinzani. 

Hata hivyo amewaomba wananchi wa Handeni Mjini kuhakikisha wanawachagua wagombea toka ccm ili waende wakawapiganie na kuwaletea maendeleo katoka maeneo yao. 

No comments:

Post a Comment

Pages