HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 21, 2020

WEEK END MBAYA KWA KANGI LUGOLA

*MAKOSA YAKE YAANGUKIA UHUJUMU UCHUMI
 TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imekamilisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola na wenzake 17.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 21, 2020 Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Brigedia Jenerali Mbungo, amesema kuwa uchunguzi wa mashitaka ya Lugola na wenzake umekamilika kwa asilimia 99.9 kwa sababu ushahidi muhimu dhidi ya tuhuma zinazowakabili tayari umeshapatikana na kilichobaki ni taratibu za uwasilishaji wa jalada hilo la uchunguzi katika ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP).  

"Ndani ya wiki moja tunatarajia kulikabidhi jalada  la uchunguzi katika ofisi ya Taifa ya Mashitaka, ni kweli tuligundua kuwa kuna matatizo na ndio maana tumefanya uchunguzi wa tuhuma hizo kwa muda wa wiki tatu.


"Uchunguzi huu naweza kuuita umefanikiwa na umefanyika kwa muda mchache na si kawaida uchunguzi kukamilika ndani ya muda mfupi kiasi hiki, kwanini tunapeleka Ofisi ya Taifa ya Mashitaka kwa sababu sheria ya Takukuru imeidhinisha makosa 23 kati ya 24 ya rushwa ni ya uhujumu uchumi ambayo ili yaendelee lazima yapate kibali cha Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP)," alisema.

No comments:

Post a Comment

Pages