Kaimu Katibu Mkuu Idara Kuu ya Maendeleo ya
Jamii kutoka Wizara Bw. Leornard Mchau (mwenye mvi) akiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi
wa Msafara wa wa kitaifa wa wa kijinsia wenye lengo la kutokomeza ukatili wa
kijinsia leo jijini Dodoma utakoanzia Mpanda mkoano Latavi tarehe 24/02/2020. Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW.
Na Mwandishi Wetu Dodoma
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii imebariki kuanza kwa Msafara wa kitaifa wa wa kijinsia
wenye lengo la kutokomeza ukatili wa kijinsia.
Akizungumza na wawakilishi wa Wizara, Wadau kutoka
Legal Services Facility, Wildaf na wasanii wa muziki wa kizazi kipya leo jijini
Dodoma Kaimu Katibu Mkuu Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bw.
Leonard Mchau amesema msafara huo umeandaliwa maalum kupeleka ujumbe wa
kupambana na ukatili wa kijinsia kuelekea maadhimisho ya kitaifa ya Siku ya
Wanawake Duniani.
Bw. Mchau amewaasa wawakilishi hao wa Msafara huo
kupeleka ujumbe huo ambao utasaidia kuendeleza mapambano ya kutokomeza vitendi
vya ukatili nchini ambavyo vimekuwa vikishamiri kila siku katika jamii.
Ameongeza kuwa Serikali imeweka mkazo katika
kuhakikisha vitendo vya ukatili wa
kijinsia vinatokomea kwa kasi ili watoto na wanawake
wanaoathirika na vitendo hivyo kuoondokana na vitendo hivyo vinavyowanyima baadhi
ya haki zao msingi.
Akizungumza kwa naiaba ya Wadau Mwakilishi wa
Shirika la LSF Bw. Joseph Magazi ameishukuru Serikali kwa kuwashirikisha waau
katika kampeni ya kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia na wameahidi
kuendxelea kusirikiana na Serikali katika mapambano hayo.
Akizungumza kwa naiaba ya Wasanii Bw. Nurdil Bilal
maarufu kama ‘Shetta’ amesema watatumia sanaa yao kufikisha ujumbe kwa jamii
kwani wao ni mmoja ya wanajamii na wanapaswa kushirikiana nayo kusaidia
kupambana kutokomeza vitendo vya kikatili katika jamii.
Msafara huu utaanzia katika mkoa wa Katavi wilaya ya Mpanda tarehe 24/02/2020 na kuendelea
hadi tarehe 05/03/2020 katika vituo vifuatavyo, Sumbawanga, Rukwa tarehe 25/02/2020
Vwawa, Songwe tarehe 26/02/2020, Mbeya Mjini tarehe 27/02/2020 Makambako, Njombe
tarehe 28/02/2020 Iringa Mjini, Iringa tarehe 29/02/2020 Tabora Mjini, Tabora
Mjini tarehe 01/02/2020 Shinyanga mjini tarehe 03/03/2020 Maswa Simiyu tarehe
04/03/2020.
No comments:
Post a Comment