Na Talib Ussi, Zanzibar
Wizara
ya Afya Zanzibar itazindua zoezi la siku kumi la kupiga dawa ya
majumbani ya kuulia viluilui vya Malaria tarehe 13 na kuendelea hadi
tarehe 27 mwezi huu.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari katika Ofisi ya kumaliza Malaria Mwanakwerekwe,
Naibu Waziri wa Afya Harusi Saidi Suleiman alisema zoezi hilo litazihusu
shehia 76 Unguja na Pemba.
Alisema
shehia zitakazopigwa dawa kwa upande wa Unguja ni 67 na Pemba ni shehia
9 ambapo zaidi ya nyumba 41,000 zitahusika katika zoezi hilo.
Alisema
baadhi ya shehia katika Wilaya zote za Unguja zitapigwa dawa na pemba
ni Wilaya ya Mkoani yenye shehia moja, Wete shehia tano na Micheweni
shehia tatu.
Naibu
Waziri alisema Wilaya za Unguja zimepatikana na mambukizi ya Malaria
kuliko Wilaya za Pemba na ndio sababu ya shehia nyingi za zitapigiwa
dawa.
Aliwataka
wananchi watakaopigiwa dawa kutoa ushrikiano kwa wapiga dawa wanapofika
majumbani mwao na kufanya maandalizi ndani ya nyumba zao na kuweka maji
kwa ajili ya kazi hiyo.
Aliwatoa
wasi wasi wananchi kuwa vijana watakaofanya kazi hiyo wamepatiwa
mafunzo maalumu ya uadilifu na hivyo wasiwe na mashaka nao.
Aliwashauri
wananchi watakaopigiwa dawa kuendeleza mikakati ya kujikinga na Malaria
kwa kutumia vyandarua vilivyowekwa dawa na kuacha tabia ya kutumia dawa
kabla ya kuthibitishwa kuwa na Malaria.
"Mkishapiguwa dawa isiwe mwisho kuchukua hadharani endeleeni na kuingia na Maleria" alisema Naibu waziri
Mkurugenzi
Kinga na Elimu ya Afya Dk. Fadhil Abdalla alisema zoezi la kupiga dawa
majumbani ni moja ya mikakati ya inayotumiwa na Wizara hiyo kupambana na
Malaria.
Alisema
kiwango cha Malaria Zanzibar bado kipo chini ya asilimia moja lakini
lengo la Wizara ni kuhakikisha maradhi hayo yanamalizika kabisa.
"Jamani tuweni making Maleria imekuja upyaa tuzisheni mikakati ya kujinga ili iondoke tena" alisema Dk. Fadhil
Mfuatiliaji
mwenendo wa maradhi ya Malaria Wahida Shirazi Hassan alisema idadi ya
kesi za maradhi ya Malaria ziliongozeka mwaka 2019 ukilinganisha na
mwaka 2018 kutoka kesi 5640 hadi kufikia 6760 ambapo wagonjwa watano
walifariki
No comments:
Post a Comment