Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi - Sospeter Magesse (kushoto),
akimkabidhi fulana 1800 Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu - Jumanne
Sagini kwa ajili ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi - Sospeter Magesse (kushoto),
akimkabidhi fualana 1800 Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu - Jumanne
Sagini kwa ajili ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi - Sospeter Magesse (kushoto),
akimkabidhi fulana 1800 Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu - Jumanne
Sagini kwa ajili ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.
Na Mwandishi Wetu, Simiyu
Wakati Mkoa wa Simiyu ukiwa mwenyeji wa maadhimisho
ya Siku ya Wanawake Duniani Kitaifa Machi 8, 2020, Benki ya NMB imenogesha
maadhimisho hayo kwa kutoa msaada wenye thamani ya Sh. Milioni 26.
Msaada huo ni pesa taslimu kiasi cha Sh. Milioni
5 pamoja na fulana zenye thamani ya Sh. Milioni 21, ambapo umekabidhiwa na
Meneja wa benki hiyo Kanda ya Magharibi Sospeter Magesse.
Akipokea msaada huo, Katibu Tawala wa Mkoa Jumanne Sagini, aliishukuru benki hiyo kwa msaada huo walioutoa ambao
alieleza utasababisha maadhimisho hayo kupendeza.
Sagini alisema kuwa NMB imekuwa benki pekee na
mdau mkubwa wa maendeleo katika Mkoa wa Simiyu, kwani kwa miaka miwili
mfululuzo imekuwa ikidhamini maazimisho ya Siku ya Wakulima Kitaifa ambayo
yamefanyika mkoani hapo.
Alisema kuwa Ofisi ya Mkoa inamshukuru Mkurugenzi
Mkuu wa Benki hiyo, kwani kila wanapowasilisha maombi ya msaada wowote kwake
amekuwa hasiti kusaidia.
“ Tunajua NMB imeshiriki mambo mengi kwenye Mkoa
wetu ya maendeleo, kwenye Nanenane ambayo mwaka huu inafanyikia hapa kwa mara
ya tatu, NMB wamekuwa wakishiriki kudhamini kila mwaka,” alisema Sagini.
Aliongeza kuwa, maandalizi yote yamekamilika na mgeni
rasmi atakuwa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan.
Kaba ya kukabidhi msaada huo, Meneja huyo wa Kanda ametoa fulana 1800 ambazo zitavaliwa na washiriki wote wa maazimisho hayo
pamoja na pesa Sh. Milioni 5 kwa ajili ya kusaidia kukamilisha maandalizi.
Magesse alisema kuwa benki hiyo itaendelea kuwa
mshirika mkuu na mkubwa wa maendeleo katika mkoa wa Simiyu, huku akitumia
nafasi hii kuwataka wanawake kuchangamkia fursa ya mikopo midogo inayotolewa na
benki hiyo.
No comments:
Post a Comment