Makamu
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi Mheshimiwa Steven Kayogolo
akitoa maagizo ya mwisho kwa Afisa utumishi na Mwanasheria wa
Halmashauri hiyo (hawapo pichani) juu ya kutafuta vifungu vya kanuni za
kuwawajibisha watumishi wakati akifunga baraza la madiwani.
Na Mwandishi Wetu
Baraza la
Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi limeazimia kuzitumia kanuni za
utumishi wa umma zinaoelezea adhabu inyaotolewa kwa watumishi ambao
hawawajibiki ipasavyo kwa mwajiri wao katika kuhakikisha wanakusanya ushuru
kwenye maeneo yao waliyopangiwa na hatimae kuongeza mapato ya halmashauri hiyo
iliyopo Mkoani Rukwa
Kauli hiyo
imetolewa na kaimu mwenyekiti wa halmashauri hiyo Mh. Steven Kayogolo wakati
akifunga baraza hilo la robo ya pili ya mwaka wa fedha 2019/2020 na kuongeza
kuwa baraza hilo limekuwa likitumia njia kadhaa ambazo hadi sasa hazijawaletea
matunda huku mapato ya halmashauri hiyo yakiendelea kudemadema jambo ambalo
linaathiri utendaji kazi wa halmashauri hiyo.
“Kwahiyo
tutatafu kama watatu hivi “demo” tunajaribu mitambo, kwahiyo watu wakae
wajitathmini, wapo watu wanaosimamia mageti, tunataarifa tunazo ambazo watu
wanafanya udanganyifu kwenye mapato, sasa mimi nawaambia kuna mtu ataruhusu
gari iondoke, tutaikamata, tukimkamata huyo haponi, huo ndio msimamo wa halmashauri,”
Alisisitiza.
Wakati
akitoa salamu za katibu Tawala wa mkoa katika baraza hilo Afisa wa Serikali za Mitaa
wa Mkoa wa Rukwa Abinus Mgonya alisikitishwa kwa kuporomoka kwa ukusanyaji wa
mapato ya halamshauri hiyo hali ambayo ilikuwa tofauti ukilinganisha na mwaka
wa fedha wa 2018/2019 katika kipindi cha kuanzia mwezi Julai hadi januari.
Alisema kuwa
hali ya ulinganifu wa kipindi hicho siyo nzuri kwa halmashauri ya Nkasi na
kuongeza kuwa halmashauri hiyo imekuwa ya mwisho kati ya halmashauri nne za
mkoa huo ambapo Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga ikiongoza katika
ukusanyaji wa mapato ikifuatiwa na halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga, huku
Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo ikishika nafasi ya tatu.
“Halmashauri
ya Wilaya ya Nkasi kwa mwaka 2019 mwezi Februari makusanyo yalikuwa ni shilingi
1,517,348,839 sawa na 66% ya makadirio ya Shilingi 2,000,304,000 kwa mwaka 2020
hadi mwezi Januari, halmashauri ya wilaya ya Nkasi ilikuwa imekusanya shilingi
919,830,000 na hii ni kwa mujibu wa takwimu tulizonazo pale mkoani kabla ya
halmashauri haijafanya usuluhishi wa mifumo ya matumizi na mifumo ya mapato ndio
maana sisi pale mkoani inasomeka 36.9%,” Alisema
Na kusisitiza
kuwa Halmashauri hiyo imeteremka kimapato kutoka 66% mwaka jana kipindi kama
hicho hadi kufikia 36.9% ambapo ni sawa na anguko la asilimia 30% na
kutanabaisha kuwa kutokana na anguko hilo ni dhahiri kuwa jambo linaitafuna
halmashauri hiyo na hivyo kuwataka waheshimiwa madiwani kujifanyia tathmini
Halikadhalika
alitilia makazo suala la kuziwasilisha benki fedha zote zilizokusanywa kabla ya
kupangiwa matumizi na halmashauri ili ziweze kusomeka katika Mfumo wa Taarifa
za Ukusanyaji Mapato wa Serikali za Mitaa (LGRCIS) na kuongeza kuwa hadi Januari
31, fedha ambazo zilikuwa mikononi mwa wakusanya mapato na hazijawasilishwa
benki kwa halmashauri ya Wilaya ya nkasi ni shilingi 101,947,971 na baada ya
kufanyika usuluhishi kwa mwezi Februari shilingi 73,954,991 zimeingizwa benki
na hivyo kuwataka kuelekeza nguvu katika vyanzo vinavyochangia Zaidi mapato.
Manispaa ya
Sumbawanga kwa mwaka 2019 mwezi Februari makusanyo yalikuwa shilingi bilioni 2.1
sawa na 98.1% ya makadirio ya shilingi bilioni 2.2 na Januari, 2020 imekusanya
shilingi bilioni 1.7 sawa na 73% ya makadirio ya shilingi bilioni 2.4,
Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga kwa mwezi Februari 2019 makusanyo yalikuwa shilingi
milioni 801 sawa na 35% ya makadirio ya shilingi bilioni 2.3 na Januari 2020
imekusanya shilingi bilioni 1.3 sawa na 54% ya makadirio ya shilingi bilioni
2.3 na Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo kwa mwezi Februari 2019 makusanyo
yalikuwa ni shilingi milioni 720.9 sawa na 36.05% ya makadirio ya shilingi
bilioni 2. Na Januari 2020 imekusanya shilingi milioni 865.2 sawa na 46% ya makadiririo
ya shilingi bilioni 1.8.
No comments:
Post a Comment