Mkurugenzi Idara ya
Uratibu wa shughuli za Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe akimkabidhi
Mkuu wa wilaya ya
Rufiji, Mhe. Juma Njwayo, misaada,
ikiwa ni magodoro, mikeka, sabuni, vyandarua na ndoo, kwa ajili ya
waathirka wa maafa ya mafuriko wilayani humo, tarehe 23
Machi, 2020.
Mkurugenzi Idara ya
Uratibu wa shughuli za Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe akiongozwa
na Mbunge wa Jimbo la Rufiji, Mohamed Mchengerwa kukakagua maeneo
yaliyoathirika na maafa ya mafuriko katika kata ya Muhoro kijiji cha Shela
tarehe 23 Machi, 2020, takribani Watu
elfu ishirini wameathirika na maafa
hayo.
Na Mwandishi Wetu
Kufuatia miundombinu ya
barabara, shule na Zahanati kuathirika kutokana na maafa ya mafuriko wilayani
Rufiji. Kamati za Usimamizi wa maafa za wilaya hiyo zimeshauriwa kuchukua hatua
za haraka katika kukabiliana na maafa hayo kwa kurejesha hali ya kawaida ya
miundombinu iliyoathirika na maafa hayo katika kata zote 13 za wilaya hiyo.
Kata ya Muhoro na Chumbi ni miongoni mwa kata
zilizoathirika sana na maafa hayo, ambapo kwa sasa madaraja matatu yaliyopo
barabara ya Nyamwage- Utete inayoelekea makao makuu ya wilaya hiyo tayari
yameathirika, Daraja lililopo kwenye barabara ya kuelekea Mradi wa kufua Umeme
wa Mwalimu Nyerere nalo limeathirika pamoja na Daraja la Mkapa nalo limeanza
kupata athari ya mafuriko hayo.
Akiongea mara baada ya
kukagua athari za maafa na kukabidhi
misaada kwa waathirika wa maafa hayo tarehe 23 Machi 2020, Mkurugenzi Idara ya
Uratibu wa shughuli za Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe, ameeleza
kuwa Kamati za Usimamizi wa kuanzia
ngazi ya kijiji hadi wilaya, kwa mujibu wa Sheria ya Usimamizi wa maafa Na. 7 ya mwaka 2015
zinawajibika kutekeleza operesheni za dharura.
“Nimezishauri kamati za usimamizi wa maafa katika wilaya hii kuwa na mipango ya
muda mfupi ya kuhakikisha barabara zinapitika kipindi chote ili wananchi
wasishindwe kutumia miundombinu hiyo, kwani zipo barabara zinaunganisha mikoa ya
kusini na zipo barabara zinawasaidiia wananchi kuweza kuzifikia huduma za
kijamii”amesisitiza Kanali Matamwe.
Awali akiongea mara baada ya kupokea misaada
kutoka kwa Idara ya Uratibu wa maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Mkuu wa wa wilaya
hiyo, Mhe. Juma Njwayo amefafanua kuwa
misaada hiyo itakuwa ni msaada mkubwa kwa kuwa hadi sasa wapo watu zaidi ya elfu
ishirini wameathirika na maafa hayo kwa kuwa zidi ya nyumba mia moja
zimezingirwa na maji.
“Tunaishukuru Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kutuletea
Magodoro, Mikeka, Vyandarua, Ndoo na Sabuni na naamini kamati za maafa zitawajibika
kugawa vifaa hivi kwa mujibu wa taratibu za menejimenti ya maafa. Wilaya
tunaendelea na kukabiliana na maafa kwa
kaya takribani elfu sita, kama
tulivyoshauriwa kuhusu miundombinu, kwa kushirikiana na TANROADS tunaendelea
kwa kasi kuchukua hatua za kurejesha miundombinu yote iliyo athirika ”
Amesisitiza Mhe. Njwayo.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Rufiji, Mhe. Mohamed
Mchengerwa, ameeleza kuwa tangu maafa ya mafuriko yatokee wilayani humo, wamekuwa
wakipata ushirikiano wa kutosha kutoka kwa Ofisi hiyo, kupitia Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
mwenye dhamana ya masuala ya maafa Mhe. Jenista Mhagama, ambapo amekuwa akiwatuma
wataalamu na kufika kwa wakati kwa ajili ya kuzisaidia kamati za usimamizi wa maafa.
“Wananchi wa Rufiji wanafarijika sana kwa jinsi
serikali yao inavyowajali, tunatambua mafuriko yamewaathiri sana ikiwemo na
kuharibika kwa vyakula vyao, tunaomba
mtuletee mbegu ama chakula cha bei nafuu na wananchi hawataki chakula cha
bure, sisi tunataka tufanye kazi na tukipata mbegu tutafanya kazi ya kilimo
mara mafuriko yakiisha” amesisitiza , Mhe. Mchengerwa.
Kwa mujibu wa Taarifa ya Mamlaka ya Hali hewa
iliyotolewa mwezi Februari mwaka huu imeeleza kuwa kutakuwa na mvua za juu ya
wastani katika eneo kubwa la nchi kati ya mwezi Machi hadi mwezi Mei, mwak huu,
ambapo mvu ahizo zilitarajiwa kuanza kati ya wiki ya kwanza au ya pili ya mwezi
Machi na kutaraji akumaliziaka kati ya wiki ya kwanza au ya pili yamwezi Mei.
Hivyo kutokana na mvua hizo wananchi hawanbudi kuchukua tahadhari za athari za
mvua hizo.
No comments:
Post a Comment