Msanii Ezra Msiliova ' Eze Nice akiwa kwenye pozi wakati wa kutengeneza
moja ya video za nyimbo zake mbili za Tanzania ya Magufuli na Asas.
NA DENIS MLOWE, IRINGA
MSANII wa muziki wa bongo fleva anayekuja kwa kasi kutoka Nyanda za Juu Kusini mwenye makazi yake mkoani Iringa, Ezra
Msiliova ' Eze Nice' ametoa wito kwa wadau wa muziki huo kuzipokea kwa
nguvu zote nyimbo zake mbili anazotarajia kuziachia hivi karibuni.
Akizungumza
na Mwanahabari, Eze Nice, alisema kuwa nyimbo hizo mbili ni zawadi tosha
kwa Rais John Magufuli na mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM mkoa wa
Iringa, Salim Abri 'Asas' kwani amezipa majina Magufuri na Asas ikiwa ni
vile ambavyo wameweza kufanya makubwa kwa maendeleo ya nchi na mkoa wa
Iringa kwa ujumla.
Eze
Nice ambaye amejichukulia maarufu mkoani Iringa kwa kuwa na nyimbo
mbalimbali za kuhamasisha maendeleo na nyingine nyimbo za siasa amekuwa
msanii wa kwanza kutoka mkoani hapa kuweza kuimba wimbo wa kumsifia
Magufuli na Salim Abri kwa kuona wanastahili sifa hivyo kutoa zawadi za
nyimbo hizo kwao.
Alisema
kuwa wimbo huo wa kwanza unajulikana kwa jina la Magufuli ambao
ameelezea kwa undani kazi zilifanywa na Rais kwa kipindi hiki na wimbo
wa pili ni zawadi kwa Salim Abri ambaye amekuwa mdau mkubwa wa maendeleo
kwa mkoa wa Iringa hivyo ili kuwaenzi kwao ametunga nyimbo hizo.
Alisema
kuwa nyimbo hizo ambazo zimefanywa chini ya mzalishaji yeye mwenyewe
kwenye studio .New Record ya mjini Iringa zinatarajia kuwa kali kwani
ziko katika mahadhi ya rumba na nzuri kwa ajili ya kucheza na kusikiliza
ujumbe uliotolewa.
"Mwandishi
nikwambie kitu hawa watu wamefanya makubwa sana kwa tanzania na mkoa wa
wetu Rais wetu kafanya yake Tanzania na kwa upande wa Mnec Salim Asas
kwa mkoa wa Iringa kafanya mengi sana kwa kweli hivyo zawadi hii nawapa
wao kila mmoja kwa kuwa na wimbo wake," alisema
Alisema
kuwa nyimbo zote zinafanyiwa video na Shama Kilasi ambaye amekuwa
akifanya video za wasanii wengi wa Nyanda za Juu Kusini na anatarajia
baada ya wiki mbili au tatu zitatoka na watu waweze kuziona ubora wake
na ujumbe uliomo kwenye nyimbo hizo.
Aidha alisema kuwa kwa upande wake kwa sasa ataachia wimbo mmoja mmoja hadi pale ambapo jamii itamtambua
vyema na kutoa albamu kali ambazo zitaheshimika nchini.
Aidha Eze Nice alivishukuru vyombo vya habari kwa kuweza
kumsimamia katika kazi zake zinaonekane kwa kuzipiga au kumtolea habari zake na kutoa wito kwa wasanii wengine kutokata tamaa
kwa kuwa Sanaa yoyote inahitaji sana nidhamu, heshima na uvumilivu ili kuweza
fikia malengo.
Alisema kuwa malengo yake
kuwa msanii mkubwa ambaye ataleta mabadiliko makubwa katika Sanaa ya muziki
akiwa chini ya kampuni hiyo kwa kuwa malengo yapo na nia anayo katika kufikisha
muziki mbali Zaidi kuliko ilivyo sasa.
Alisema kuwa amejipanga
vyema kuweza kukabiliana na changamoto zilizoko katika Sanaa ya muziki wa bongo
fleva akiwemo baadhi ya radio kuchagua wasanii na kuacha kucheza nyimbo nzuri
za wasanii wanaibuka miaka ya hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment