HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 24, 2020

Katibu Mwenezi Chadema aomba ridhaa ya kuteuliwa


Na Asha Mwakyonde

KATIBU Mwenezi wa Kata ya Kivule kupitia  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bihimba Mpaya amesema kuwa tayari ameshakiomba chama chake kimpatie ridhaa ya kugombea nafasi ya udiwani katika Kata hiyo iliyopo Jimbo la Ukonga jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Habari Mseto Blog jijini Dar es Salaam Machi 22, 2020, Mpaya ambaye pia ni Mwenyekiti wa tawi la kivule kupitia chama hicho amesema aligombea nafasi hiyo mwaka 2017 katika uchaguzj mdogo uliofanyika katika mitaa saba ya Kata hiyo baada mbunge wa Ukonga Mwita Waitara kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mpaya amesema katika uchaguzi huo mdogo alipata kura 767 dhidi ya 866 za mgombea wa CCM ambapo hazikutosha kumpatia ridhaa ya kuongoza mtaa wa Kivule.

"Mwaka2019 niligombea tena nafasi ya uenyekiti wa serikali ya mtaa lakini wapinzani tulijiondoa katika uchaguzi huu ,"amesema Mpaya.

Ameongeza kuwa  kwa muktadha huo anakiomba chama cheke kumwamini na kumpatia ridhaa ya kugombea nafasi ya udiwani.

Mpaya ameeleza kuwa amejiunga na chama hicho cha chadema tangu mwaka2014 na kwamba ni mwanachama mwenye kadi namba 2599122.

No comments:

Post a Comment

Pages