Mkurugenzi wa Masoko TBL, Doreen Tumubeebire
(kushoto) na Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, Irene Mutiganzi wakiteta
jambo huku wakifuatilia mbio za Kilimanjaro Premium Lager Marathon 2020
zilizofanyika Mjini Moshi hivi karibuni.
Na Mwandishi Wetu
SHIRIKISHO la Riadha Tanzania (RT), limeipongeza kampuni
ya Bia Tanzania (TBL), kupitia kinywaji chake cha Kilimanjaro Premium Lager kwa
mchango wao uliotukuka katika uhai wa mbio maarufu za Kilimanjaro Marathon.
Mbio za Kilimanjaro Marathon zilifanyika Machi Mosi mwaka huu,
Moshi mkoani Kilimanjaro zikiwa zinatimiza miaka 18 tangu kuanzishwa kwake.
Akizungumzia mbio hizo, Makamu wa Kwanza wa Rais RT-Utawala,
William Kallaghe, ambaye alimwakilisha Rais wa shirikisho hilo, Anthony Mtaka,
alisema mbio hizo hivi sasa zimekuwa kubwa na nembo ya Taifa, lakini hasdi
kufikia hapa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager inapaswa kupongezwa, kwani
imekuwa mdau mkubwa kwa miaka yote hiyo.
“Sekta ya michezo ni vigumu kupiga hatua bila udhamini, sisi
kama Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), tunapenda kupigia mfano udhamini
mfululizo wa Kilimanjaro Premium Lager, kwani wamekuwa na mbio hizi kwa miaka
yote hiyo bila kusimama,” alisema Kallaghe na kuongeza. Huu ni udhamini wa kipekee na kuigwa na wadhamini wengine.
Kallaghe, alisema Kilimanjaro Premium Lager Marathon, sasa
limekuwa ni tukio kubwa nchini lenye kugusa mataifa mbalimbali, ambayo
washiriki wake wamekuwa wakivutika kushiriki mwaka hadi mwaka huku akiongeza
kuwa tukio hili linatakiwa kuwa la kitaifa na sio la Moshi tu.
Aliwaomba wadhamini wengine, kuzidi kujitokeza kuwekeza kwenye
mchezo wa riadha, ambao hivi umekuwa na mvuto kwa watu wengi nchini.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Riadha Mkoa wa Kilimanjaro (KAAA),
Liston Metacha, alisema kama mkoa wanajivunia kuwa na tukio kubwa kama hilo na
wakidumu nalo kwa miaka 18 bila kukoma.
Metacha, alisema Kilimanjaro Marathon imekuwa na mchango mkubwa
kimichezo na kiuchumi sit u kwa Mkoa wa Kilimanjaro, bali Tanzania kwa ujumla
hususan kupitia sekta ya utalii.
Mwenyekiti huyo, aliwaomba Kilimanjaro Premium Lager na
wadhamini wengine ikiwamo kampuni ya simu ya Tigo, kuendelea kuliunga mkono
tukio hilo la kila mwaka.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Masoko TBL, Doreen Tumubeebire,
alisema wanajisikia furaha mbio kila mwaka inakua na hadi sasa inapofikisha
miaka 18 wamefikisha washiriki zaidi ya 11,000.
“Hii inaonyesha jinsi gani watu wametambua umuhimu
wa michezo, na katika kuimarisha afya zao,” alisema Doreen na kuongeza mwaka
huu wametumia zawadi Sh. Milioni 23 huku Mtanzania wa kwan za katika mbio za
Kilomita 42 wanaume na wanawake amepata Sh. Milioni 1.5 kama bonasi.
Mbio za mwaka huu, zimewezeshwa na Kilimanjaro
Premium Lage-42km, TIGO-21km, Grand Malt-5km, Maji ya Kilimanjaro, TPC Limited,
Simba Cement, Unilever, Absa Bank Tanzania Limited wakati wadhamini wa huduma
ni Kibo Palace Hotel, Keys Hotel, GardaWorld Security, Precision Air, CMC
Automobiles.
No comments:
Post a Comment