Wananchi wakipita katika maji baada ya barabara ya Mwaja kujaa maji na kufungwa na Serikali kufuatia mabwawa ya Kindai na Singidamunangi kukumbwa na mafuriko Manispaa ya Singida.
Wananchi wakipanda mtumbwi katika eneo la tukio.
Wananchi wakivushwa kwa mtumbwi.
Kibao cha tahadhari cha kufungwa kwa barabara hiyo.
Na Ismail Luhamba, Singida
MVUA zinazoendelea kunyesha mkoani SINGIDA zimekata mawasiliano ya barabara ya Mwaja na Manispaa singida.
Katika historia imejirudia ya maziwa haya mawili ya Kindai na Singidamunangi kuungana na kusababisha kukatika kwa Mawasiliano ya barabara za kwenda vijiji jirani na Manispaa ya Singida mahali ambapo wakazi wengi wanapata huduma za kijamii.
Wakizungumza na wanahabari wakazi wa Kindai pamoja na Mwawaja wamesema tangu maziwa hayo kuungana yamesababisha adha kubwa sana maana kuna makazi ya watu yamejaa maji na kusababisha wahame maeneo na kwenda kujiihifadhi kwa majirani na ndugu zetu.
Pia wameiomba Serikali kuhakikisha wanatafuta njia mbadala ya ili waweze kufika mjini SINGIDA badala ya kutumia usafiri wa mitumbwi ambao sio salama.
”Tunaomba Zimamoto waje pia kutoa elimu kwa hawa watu wetu wanaovusha hapa maana kuna akinamama wajawazito na wazee ni changamoto kwelikweli”
Akikagua hali ya barabara, Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskas Muragili amesema hali ya barabara ya Manispaa hadi Mwaja sio salama kwa matumizi ya watu kupita ndio maana tumechukuwa hatua ya kuifunga mpaka hapo mvua zikaoacha kunyesha na maji kupunguwa.
Muragili amewataka wananchi hasa watembea kwa miguu kuacha kabisa kupita kwenye barabara hiyo badala yake watumie ile inayopitia VETA na Mwaja ambayo inapitika vizuri.
No comments:
Post a Comment