Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu,
akizungumza jambo kuhusiana na mikakati ya serikali ya awamu ya tano ya kuweka
mipango ya kuunganisha nishati ya umeme wa gesi asilia katika viwanda vipya 50
wakati wa ziara ya Kamati ya kudumu ya bunge ya nishati na madini ambayo
ilifanya ziara yake ya kikazi ya kutembelea baadhi ya viwanda vilivyopo katika
Wilaya ya Mkuaranga. (Picha na Victor Masangu)
Badhi ya wabunge wanaounda kamati ya nishati na
madini wakati wanaingia katika kiwanda cha kuzalishia chuma cha Lodhia ikiwa ni
moja ya ziara yao ya kikazi kwa ajili ya kuijionea shughuli mbali mbali
zinazofanywa na wawekezaji pamoja na kubaini changamoto zao, wa kati kati ni
Mbunge wa Jimbo la Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa.
Kaimu mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya
nishati na Madini Vedastus Matayo akipokea maelekezo kutoka kwa mmoja wa
viongozi wa kiwanda cha kuzalishia chuma cha Lodhia kilichopo kata ya Kisemvule
wakati wa ziara ya kamati hiyo ilipokwenda kwa ajili ya kujionea shughuli mbali
mbali za uzalishaji kiwandani hapo.
Mwonekano wa mtambo maalumu wa kuzalishia nishati
ya umeme wa gesi asilia ambao umefunngwa na shirika la TPDC katika kiwanda hicho cha
ku.zalishia chuma pamoja na kutengenezea
mabomba ya maj wakati wa ziara hiyo ya kamati ya bunge ya nishati na
madini
Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Lodhia Haruni Lodhia ambacho kinajihusisha na uzalishaji
wa kutengeneza Nondo pamoja bidhaa zingine mbali mbali akizungumza mbele ya
wajumbe kamati ya bunge ya nishati na
madini hawapo pichani ilipofanya ziara
ya kikazi ya kutembelea kiwanda hicho.
Mmoja wa wakurugenzi wa kiwanda cha Lodhia ambacho
kinajishighulisha na uzalishaji wa bidhaa mbali mbali ikiwemo chuma,
akiwaonyesha wajumbe wa kamati ya bunge ya nishati na madini jinsi ya kiwanda
hicho kinavyofanya kazi pamoja na kuwaelezea changamoto mbali mbali
zinazowakabili ili kuziwasilisha kwa serikali zifanyiwe kazi.
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya bunge ya nishati na
madini wakiwa na viongozi mbali mbali wa kiwanda hicho wakitembezwa katika
maeneo mbali mbali ili kuweza kujionea mwenendo mzima wa vyuma chakavu
vinavyoyayushwa na kutengenezwa Nondo mpya kwa ajili ya utekelezaji wa miradi
mbali mbali ikiwemo ile ya serikali.
Victor Masangu, Mkuranga
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, amesema kwamba katika kutimiza azma ya Tanzania kuwa na
uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 serikali imedhamilia kusambaza na kuwaunganishia
nishati ya umeme wa gesi asilia katika viwanda vipya vipatavyo 50 ambavyo vimepitiwa na bomba la gesi ikiwemo
Mkoa wa Dar es Salaam Pwani pamoja na Mtwarana kuongeza gharama za umeme zitashuka
pindi mradi wa bwawa la umeme mwalimu nyerere utakapomalika Juni 2022 na
kuzalisha mega wati 2115.
Mgalu aliyasema hayo
wakati wa ziara ya kikazi ya kamati ya
kudumu ya bunge ya nishati na Madini ambayo yameifanya kwa lengo la kutembelea baadhi ya viwanda
vilivyopo Wilayani Mkuranga Mkoa wa Pwani ambavyo vinajiendesha kwa kutumia nishati ya
umeme ikiwa pamoja na kuzungumza na wawekezaji ili kubaini changamoto
wanazokabiliana nao na kuzitafutia ufumbuzi.
Naibu
Waziri huyo alibainisha kwamba kwa sasa serikali ya
awamu ya tanoi mpango wake mkubwa ni kuhakikisha inasambaza na
kuviunganishia
viwanda mbali mbali nishati ya umeme ili viweze kutimiza malengo ya azma
y
serikali ya kuwa na uchumi wa kati pamoja na kutoa fursa mbali mbali za
ajira kwa vijana ambao ni wazalendo lengo ikiwa waweze kujikwamua na
wimbi la
umasikini.
“Mpango wetu wa serikali licha ya kuwa bado kuna baadhi ya
maeneo ya viwanda hayajafikiwa na nishati ya umeme lakini kwa sasa kupitia
nishati ya gesi asilia tuna mpango wa kuviunganishia viwanda vipya vipatavyo 50
ambavyo vipo katika Mikio ya Dar es Salaam, Mtwara pamoja na Mkoa wa Pwani
hivyo juhudi za makusudi bado zinaendelea kwa hiyo viwanda ambavyo vinapitiwa
na bomba kubwa la gesi vitaweza kunufaika.
Aidha Naibu Waziri huyo alifafanya kwamba pindi mradi wa
umeme wa bwawa la Malimu Nyerere uliopo Wilayani Rufiji utakapokamilika utaweza
kuwa ni mombozi mkubwa kwa wawekezaji wa viwanda vidogo, vya kati na vile
vikubwa kutoka maenne mbali mbali sambamba na kuwaunganishia wananchi wengine
pamoja na taasisi za serikali na sizozo
za serikali.
Katika hatua nyingine Mgalu ameipongeza kamati ya kudumu ya
bunge ya nishati na madini kwa kuweza kwenda kutembelea katika kiwanda cha
kuzalisha chuma pamoja na mabomba ya maji ili kuweza kubainichangamoto mbali
mbali ambazo zinawakabili wawekezaji na hatimaye kuweza kuzitafutia ufumbuzi wa
kudumu ambao utasaidia kutimiza azma ya serikali ya kuwa na uchumi wa kati
kupitia viwanda hivyo.
Kwa upande wake Kaimu
mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya nishati na Madini Vedastus
Matayo alibainisha kwamba ujenzi wa kiwanda hicho utaweza kuipunguzia serikali gharama kubwa ambazo
zimekuwa zikitumia kwa ajili ya kuagiza baadhi ya Nondo kutoka nje ya nchi
hivyo amempongeza mwekezaji huyo kwa kuwekeza katika Wilaya ya Mkuranga kwani kumesaidia vijana
zaidi ya 1 300 kupata fursa ya ajira.
“Sisi kama kamati kwa kweli tunapenda kumpongeza mwekezaji
huyo kwa kuweza kuwekeza katika Wilaya ya Mkuranga ambayo ipo katika Taifa letu
ya Tanzania hii ni hatua nzuri ambayo ameifanya na kwa sasa anazalisha bidhaa
mbali mbali kwa kutumia nishati ya umeme wa gesi asilia hivyo kutaweza kuleta mabadiliko
chanya ya kimaendeleo kwa wananchi wenyewe pamoja na wale wawekezaji wa ndani
na nje ya nchi,”alibainisha Matayo
Aidha Matayo katika hatua nyingine alibainisha kuwa Kamati ya
bunge ya nishati ya kudumu ya nishati na madini ilibaini
kuwepo kwa urasimu na ucheleweshaji wa vibali kutoka kwa baaadhi ya mamlaka
zinazohusika kwa wawekezaji wa sekta ya viwanda pamoja na gharama ya nishati ya
umeme kuwa ni kubwa hivyo hivyo watayachukua mapendekezo hayo kwa ajili ya
kuyawasilisha bungeni ili serikali iweze kuyatafutia ufumbuzi wa kudumu.
Pia alisema kuwa mapendekezo pamoja na changamoto mbali
mbali ambazo wamekutana nazo katika kiwanda hicho ikiwemo na maeneo mengine
ambayo tayari wameshayapitia watayawasilisha serikalini ili yaweze kufanyiwa
kazi ikiwemo na kutilia mkazo katika suala la usumbufu mkubwa wanaoupata
wawekezaji pindi wanapohitaji kuagiza matilio mbali mbali kutoka nje ya nchi
kwa ajili ya kutengeneza bidhaa zao.
Awali akitoa taarifa
mbele ya Kamati ya nishati na madini Mkurugenzi mtendajiwa wa kiwanda hicho cha
kuzalisha chuma Haluni Lodhia amebainisha kwamba hapo awali walikuwa
wanakabilia na changamoto kubwa ya ukosefu wa nishati ya umeme wa uhakika
pamoja na miundombinu ya barabara,ambapo ameipongeza serikali ya awamu ya tano
kupitia Shirika la maendeleo ya Petroli
Tanzania (TPDC) kwa litafutia ufumbuzi suala hilo na hatimaye kuanza
utekelezaji wa kuzalisha bidhaa mbali mbali, ikiwemo Nondo, mabomba ya maji na
bodi za jasi.
No comments:
Post a Comment