Katibu
Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (kulia)
akimpongeza Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Utawala na Rasilimaliwatu, Mkoa wa
Shinyanga, Bw. James Bwana kwa kuwezesha kupatikana kwa vitendea kazi vya kielektroniki
toka Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Umoja wa Mataifa (UNDP) mara baada ya
Katibu Tawala huyo kukabidhi vitendea kazi hivyo leo katika ukumbi wa Ofisi ya
Rais, Utumishi, Mtumba jijini Dodoma.
Katibu
Tawala Msaidizi Sehemu ya Utawala na Rasilimaliwatu, Mkoa wa Shinyanga, Bw.
James Bwana akitoa maelezo ya vitendea kazi vilivyotolewa na UNDP kwa Katibu
Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro
(kulia) katika ukumbi wa Ofisi ya Rais, Utumishi, Mtumba jijini Dodoma leo.
Katibu
Tawala Msaidizi Sehemu ya Utawala na Rasilimaliwatu, Mkoa wa Shinyanga, Bw.
James Bwana, akionyesha nyaraka zenye orodha ya vitendea kazi vilivyotolewa na
UNDP kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt.
Laurean Ndumbaro (kulia).
Kaimu
Mkurugenzi wa Kitengo cha Ununuzi na Ugavi, Ofisi ya Rais, Utumishi, Bw. Victor
Ngole, akipokea nyaraka leo toka kwa Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Utawala
na Rasilimaliwatu, Mkoa wa Shinyanga, Bw. James Bwana zinazoonyesha orodha ya vitendea
kazi vilivyotolewa na UNDP. Anayeshuhudia ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro.
Vitendea
kazi vya kielektroniki vilivyotolewa na UNDP kwa ajili ya kuboresha utendaji
kazi wa watumishi wa watumishi wa Ofisi ya Rais, Utumishi vikishushwa leo kwa
ajili ya makabidhiano rasmi katika ofisi hiyo, Mtumba jijini Dodoma.
James Mwanamyoto -
Dodoma
Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, katika kuboresha
utendaji kazi na utoaji wa huduma bora kwa wananchi, imepokea vitendea kazi vya
kielektroniki toka Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Umoja wa Mataifa
(UNDP).
Vitendea
kazi vilivyopokelewa ni Kompyuta saba (7), “printer”
10 na kompyuta mpakato tatu (3) vyenye thamani ya shilingi 45,919,500/=.
Akipokea
vitenda kazi hivyo leo toka kwa Bw. James Bwana, Katibu Tawala Msaidizi Sehemu
ya Utawala na Rasilimaliwatu, Mkoa wa Shinyanga, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro amemshukuru kwa jitihada
zake za kuwezesha upatikanaji wa vitendea kazi hivyo toka UNDP. Awali, James
Bwana alikuwa Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Ushirikiano wa Kimataifa, Ofisi ya
Rais, Utumishi.
“Nakupatia
kompyuta mpakato moja itakayokuwezesha kutekeleza majukumu yako ikiwa ni sehemu
ya kutambua mchango wako katika upatikanaji wa vitendea kazi hivyo.” Dkt.
Ndumbaro amesisitiza.
Aidha,
Dkt. Ndumbaro ameishukuru UNDP kwa kutoa vitendea kazi hivyo vitakavyosaidia kuongeza
ufanisi wa kiutendaji kwa watumishi wa ofisi yake.
Kwa
upande wake, Bw. Bwana, amemshukuru Dkt. Ndumbaro kwa kumpatia ridhaa ya
kufanya mchakato wa upatikanaji wa vifaa hivyo toka UNDP kwa lengo la kuboresha
utendaji kazi wa Watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora.
No comments:
Post a Comment