HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 01, 2020

Restless Development yawafunda waandishi kuhusu FP, ukatili wa kijinsia

 Ofisa Mradi wa Tutumize Ahadi unafadhiliwa na Shirika la Restless Development, Anna Winston, akizungumza na waandishi wa habari walioshiriki mafunzo ya Uzazi wa Mpango (FP) na ukatili wa kijinsia yaliyofanyika mkoani Morogoro. (Picha na Suleiman Msuya)
Mratibu Mwandamizi wa Mradi wa Tutimize Ahadi unafadhiliwa na Shirika la Restless Development, Anna Winston akizungumza na waandishi wa habari walioshiriki mafunzo ya Uzazi wa Mpango (FP) na ukatili wa kijinsia yaliyofanyika mkoani Morogoro.


Na Suleiman Msuya, Morogoro

WAANDISHI wa habari wameshauriwa kutembelea maeneo ya vijijini ili kuweza kuandika namna Serikali inavyotekeleza sera zake za usawa wa kijinsia na Uzazi wa Mpango (FP).

Ushauri huo umetolewa na Mtaribu Mwandamizi wa Mradi wa Tutimiza Ahadi, unaotelezwa na Shirika la Restless Development Sima Bateyunga, wakati akizungumza na waandishi wa habari walioshiriki mafunzo ya siku moja kuhusu masuala ya usawa wa kijinsi na FP.

Bateyunga alisema Shirika la Restless Development limekuwa likijishughulisha na kutoa elimu kuhusu usawa wa kijinsia na uzazi wa mpango kwenye mikoa mbalimbali ikiwa ni kuunga mkono mipango ya Serikali na mikataba ya Kimataifa kwenye eneo hilo.

Alisema waandishi wa habari wakipata taarifa sahihi kutoka kwa jamii moja kwa moja watabaini namna ambavyo Serikali imefanikiwa katika maeneo hayo muhimu na wapi imekwama na kuyaripoti.

"Serikali inatekeleza sera kuhusu FP 2020 na usawa wa kijinsia ambao upo kwenye lengo la tano la Maendeleo Endelevu SDG 5, haya yataoneka iwapo waandishi wa habari watatoa taarifa sahihi ya hali ilivyo na sio kusubiri taarifa za Restless Development," alisema.

Mratibu huyo alisema kiuhalisia Serikali imepiga hatua kiasi fulani kwenye maeneo hayo hivyo kuitaka iongeze juhudi ili kwenda kwenye malengo tarajiwa.

Bateyunga alisema kwa sasa eneo la uzazi wa mpango, uwezo wa kutoa taarifa kuhusu matukio ya ukatili wa kijinsia, watu wanaofikiwa ndani ya saa 72 na vijana ambao wanapata taarifa kwa wakati kuhusu changamoto za ujana wao umepiga hatua.

Alisema zipo jitihada za Serikali katika kuongeza Bajeti kwenye eneo hilo lakini bado uhitaji ni mkubwa.

"Nitumie nafasi hii kuyaomba makundi yote hasa ya waliopo vijijini kutafuta taarifa sahihi kwenye maeneo husika na sisi Restless Development tutaendelea kutoa elimu ili Tanzania itimize malengo iliyojiwekea," alisema.

Bateyunga alisema Tanzania ikiweza kugusa eneo hilo kwa kina utegemezi wa kulea, elimu na changamoto zingine zitataluliwa.

Kwa upande wake Ofisa Maradi wa Tutimize Ahadi, Anna Winston, alisema mradi huo umelenga kutafuta takwimu sahihi ya changamoto ya FP na unyanyasaji wa kijinsia.

"Mfano kati ya wasichana 10 wawili wanapata mimba na watatu wanapata ikatili wa kijinsia kati ya 10 hivyo tatizo ni kubwa ila Restless Development kwa kushirikiana na wadau wengine watafanikiwa kupunguza hali hiyo," alisema.

Winston alisema ahadi ya Serikali ni kuwepo vituo vya uzazi wa mpango na huduma rafiki kwa vijana ambapo wao wameshafikia zaidi ya vijana 1,000 katika wilaya ya Bahi, Kilolo, Irjnga DC na Manispaa ya Dodoma.

Alisema wanatarajia Serikali itaongeza nguvu kubwa kutatua changamoto hizo kwa kupitia vikao vya maamuzi kuanzia ngazi ya chini hadi juu.

Aisha, aliwataka wananchi kutoa taarifa kuhusu matukio ya ukatili wa kijinsia ili vyombo vya Serikali viweze kuchukua hatua stahiki.

No comments:

Post a Comment

Pages