HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 12, 2020

TCRA yatoa Elimu ya Mawasiliano kwa Viongozi wa Dini mkoani Kagera

 Katibu Tawala wa Mkoa Kagera - Prof. Faustine  Kamuzora ,akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa  wa Kagera katika ufunguzi wa semina ya kuelimisha kamati ya Amani ya mkoa wa Kagera  jinsi ya kujikinga wanapotumia huduma za Mawasiliano ikiwa ni Muendelezo wa Kampeni ya SIRUBUNIKI “Mjanja haingizwi Chaka” inayoendelea  nchini iliyofanyika Mkoani Kagera
 Mkuu wa Kanda ya Ziwa wa TCRA Francis Mihayo akizungumza katika semina ya Kamati ya Amani Mkoa Kagera kuhusiana na Kampeni ya TCRA ya Sirubuniki Mjanja haingizwi Chaka.
 Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Polisi Joshua Mwangasa akizungumza kuhusiana na makosa ya mitandao viongoz dini  Mkoa was Kagera katika Kampeni ya Sirubuniki Mjanja haingizwi Chaka
 Sheikh wa Mkoa wa Kagera na Mwenyekiti wa Kamati ya Amani Mkoa huo  Haruna Kichwabuta  akizungumza katika semina ya viongozi wa dini kuhusiana na Kampeni ya TCRA  Sirubuniki Mjanja haingizwi Chaka.
 Baadhi ya viongozi wa dini wa Mkoa wa Kagera.
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Profesa Faustine Kamuzora akiwa picha ya pamoja  na Kamati ya amani Mkoa wa Kagera.


 Na Mwandishi Wetu, Kagera

Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Profesa Faustine Kamuzora ameiopongeza Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuja kwa  kampeni ya sirubuniki Mjanja Haingizwi Chaka.

Profesa Kamuzora ameyasema hayo wakati  akifungua semina ya Kamati ya Amani Mkoa wa Kagera  iliyoandaliwa na TCRA kutoa Elimu ya Kujikinga na uhalifu unapotumia  huduma za mawasiliano.

Katibu Tawala Profesa Kamuzora amewaomba  viongozi  wa dini  waunge  mkono  serikali kupitia  TCRA kueneza  elimu ya Mawasiliano.

 Amesema   viongozi wa dini Wana  wanaumini wengi hivyo ni rahisi  kufikisha elimu hiyo. "Ninaamini  viongozi wa Dini mkivalia  njuga  basi watu wataweza kujikinga na uhalifu wakati wa wanaotumia huduma za mawasiliano"Amesema Profesa Kamuzora.

Naye Mkuu wa Kanda ya Ziwa Francis Mihayo amesema viongozi wa dini ni minutes katika kuwa daraja ya kufikisha taarifa kwa haraka na watu.

Mihayo amesema  kuwa semina ya viongozi wa dini itazaa matunda kwa wananchi kuwa na uelewa namna ya kutumia mawasiliano.

Aidha  amesema kuwa Kanda ya Ziwa itaendelea kutoa Elimu ya Mawasiliano katika Kujikinga na uhalifu unapotumia huduma za mawasiliano.

 Kampeni  ya Sirububiki Mjanja haingizwi chaka  inalenga kuzifikia kamati za Amani za mikoa yote ya Tanzania
 Kamati za Amani za mikoa ni kamati za viongozi wa dini na madhehebu  mbalimbali ambazo zimeundwa kwa lengo  la kujenga  maridhiano kwa watu wa dini mbalimbali

Nae Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa TCRA Mabel Masasi amesema kuwa wanafikia makundi yote katika Kampeni ya Sirubuniki  Mjanja Haingizwi Chaka.

Amesema wakati amefikia wa kutumia mawasiliano kwa kulinda usalama wa nchi  pamoja na wanaotumia mawasiliano bila kufuata sheria na taratibu mkono wa sheria utawakuta.

No comments:

Post a Comment

Pages