Mkuu
wa Mkoa wa Songwe, Brig. Jen. Nicodemus Mwangela (aliyevaa miwani), akikagua
orodha ya bidhaa ambazo zimetolewa na Mamlaka ya Mapato (TRA) kutokana na kuwa
zimekamatwa kwa njia za njia za magendo na wamiliki hawakujitokeza.
Simenti iliyokamatwa
kwa kuingizwa nchini kwa njia za Magendo katika Mpaka wa Tunduma ikitolewa kwa
ajili ya kupelekwa katika shule za sekondari za Mkoa wa Songwe.
Na Mwandishi Wetu
Mamlaka ya Mapato
Nchini (TRA) Mkoa wa Songwe imegawa baadhi ya bidhaa zilizo kamatwa kwa kuingizwa
Nchini kupitia mpaka wa Tunduma kwa njia za Magendo ili kukwepa ushuru.
Akipokea bidhaa hizo
kutoka Kwa Kaimu Meneja TRA Mkoa wa Songwe, Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen.
Nicodemus Mwangela amesema bidhaa hizo zinapelekwa katika shule za Sekondari za
Mkoa wa Songwe ili ziweze kuwasaidia wanafunzi.
“Nimepokea simenti
mifuko 192, mafuta ya kupikia ndoo 37 na sukari katoni 70 ambavyo vyote
navielekeza katika shule za Sekondari
ili vikasaidie huko.” , amesema Brig. Jen. Mwangela.
Amesema mifuko 100 ya
simenti ameelekza ipelekwe Wilaya ya Momba ambapo kuna ujenzi wa shule ya
sekondari ya Wasichana kwa kidato cha tano na sita na sukari imetolewa kipaumbele
Wilaya ya Mbozi ambayo watakuwa wenyeji wa wanafunzi wa Michezo ya Umiseta.
Brig. Jen. Mwangela
amewataka Wakuu wa Wilaya kuhakikisha wanafuatilia bidhaa hizo ili zitumike kwa
malengo yaliyokusudiwa na si vinginevyo.
Naye Mkuu wa Wilaya
ya Momba Juma Said Irando ametoa wito kwa wananchi na wafanyabiashara waliozoea
kutumia njia zisizo halali kuingiza bidhaa nchini Kupitia Mpaka wa Tunduma waache
maramoja kwani kamati ya Usalama ya Wilaya yake imeimarisha doria ili kumaliza tatizo
la wakwepa kodi.
Irando amewata
wafanyabiashara kutumia njia halali pia wazingatie sheria na taratibu za
forodha ili waweze kufanya bishara halali na kuepuka hasara kwakuwa
watakamatwa.
Amesema kuwa
wafanyabiashara watambue kuwa wakikamatwa na bidhaa ambazo zimeingizwa Nchini
isivyo halali sio tu watataifishwa mali hizo bali sheria zinawataka walipe kodi
na faini ili wachangie pato la Nchi.
Irando ameongeza kuwa
Wilaya yake imepokea mifuko 100 ya simenti ambayo itasaidia katika ujenzi wa
Sekondari ya Wasichana ambayo itakuwa sekondari ya A level kwa wasichaa pekee Mkoa wa Songwe.
Kwa upande wake Kaimu
Meneja wa TRA Mkoa wa Songwe Farensi Mniko amesema walifanikiwa kukamata bidhaa
hizo kutokana na kuimarisha kaguzi mbalimbali katika Mpaka wa Tunduma pia kwa
kupata taarifa kutoka kwa wananchi mbalimbali.
Mniko ameongeza kuwa bidhaa
zilizo kamatwa zikikaa muda mrefu bila mhusika kuzichukua Kamishna wa TRA anayo
mamlaka ya kuzigawa kwa taasisi za serikali kama alivyo fanya kwa bidhaa za
simenti, sukari na mafuta alizozitoa.
Ameongeza kuwa bidhaa
hizo hukaguliwa ubora wake kabla hazijagawiwa kwa taasisi za serikali hivyo
zinakuwa salama, huku akiwasisitiza wafanyabiashara waache kupita njia zisizo
halali kwakuwa TRA imejipanga kukomesha magendo.
No comments:
Post a Comment