HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 05, 2020

BENKI YA NIC YAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI KATIKA HOSPITALI YA CCBRT

 Mkurugenzi Mkuu wa NIC Bank, Margret Karume (kushoto)  akimkabidhi vifaa mbalimbali Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Brenda Msangi kwa ajili ya wagonjwa wa Fistula waliolazwa kwenye hospitali hiyo ikiwa ni sehemu ya kusherehekea kwa pamoja maadhimisho ya wiki ya wanawake Duniani. Hafla hiyo imefanyika Hospitali ya CCBRT jijini Dar Es Salaam leo.

 
Na Mwandishi Wetu

Ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani, Benki ya NIC imeadhimisha siku hiyo muhimu kwa wanawake kwa kutembelea na kutoa misaada mbali mbali kwa wanawake wanaotibiwa ugonjwa wa Fistula hospitali ya CCBRT.

Siku ya Kimataifa ya Wanawake huazimishhwa kila mwaka kusherehekea mafanikio waliyopata wanawake katika nyanja mbali mbali kama vile kijamii, kiuchumi, kitamaduni na kisiasa.

Maadhimisho haya pia yanasaidia kupaza sauti juu ya suala la usawa wa kijinsia. Yakiwa na kauli mbiu ‘Usawa kwa Wote’, kauli hiyo inahimiza kuwa usawa siyo jambo la wanawake bali ni jambo la kibiashara. Usawa wa kijinsia ni muhimu kwa uchumi na kwa maendeleo ya jamii. Usawa wa kijinsia siyo jambo la mjadala wa siku moja ambao utaisha katika siku ya wanawake duniani bali ni suala endelevu.

Ili kusaidia jamii ambayo inatuzunguka, tumeamua kutumia siku hii kuimarisha uhusiano wet na hospitali ya CCBR. Benki yetu leo imeamua kuja hapa na kutoa misaada mbali mbali itakayowasidia wanawake wanopata matibau ya fistula hospitalini hapa,” alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Margaret Karume.

Akizunguma wakati wa kutoa misaada hiyo, mkurugenzi wa benki hiyo alisema benki yake ni moja kati ya taasisi zinazojali suala la usawa i kwenye mambo mbali mbali ikiwa ni pamoja na ajira na kuongeza kuwa pia benki hiyo inathmini jamii inayozizunguka na huzisadia katika nyanja za elimu, afya na mazingira.

“Tunafurahi kushiriki maadhimisho ya siku ya wanawake duniani pamoja wanawake hapa CCBRT. Kusaidia jamii inayotuzunguka na wanawake ni moja kati ya vipaumbele vya benki yetu.

Unapomsaidia mwanamke, humsaidii peke yake bali unasaidia jamii nzima nan chi kwa ujumla,” alisema Usawa wa kijinsia unahitaji uwezeshaji kwa wote ukilenga kutatua changamoto ya kutokuwa na maamuzi sawa na pia kumpa kila mtu nguvu na uhuru wa kuamua maisha yake.

Aliongeza kuwa watu wote wakiwa wamewezeshwa, familia zinanufaika na manufaa haya yanakwenda mpaka kwa vizazi vijavyo na familia kwa ujumla.

Benki ya NIC itaendelea kusaidia jamii katika namna mbali mbali ambazo zitamnufaisha mtu mmoja mmoja na jamii yote kwa ujumla wake,” alisema

No comments:

Post a Comment

Pages