Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Dk Augustine Mahiga na Katibu wa Wizara hiyo, Profesa Sifuni
Mchome wakimsalimia Mbunge wa Malindi, Ally Saleh walipokutana Mkoani Morogoro kuhudhuria
warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) kwa
kushirikiana na taasisi ya Haki Maendeleo.
Mchome wakimsalimia Mbunge wa Malindi, Ally Saleh walipokutana Mkoani Morogoro kuhudhuria
warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) kwa
kushirikiana na taasisi ya Haki Maendeleo.
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Jaji (Mst.) Mathew Mwaimu akiwasilisha taarifa ya THBUB kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria katika warsha iliyoandaliwa Mkoani Morogoro na THBUB kwa kushirikiana na Haki Maendeleo . Katikati ni Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Emmanuel Mwakasaka, wa kwanza kushoto ni Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Dk. Augustine Mahiga.
Kaimu Katibu Mtendaji wa THBUB, Hajjat Fatuma Muya akisisitiza jambo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria waliohudhuria warsha warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) kwa kushirikiana na taasisi ya Haki Maendeleo Mkoani Morogoro.
Na Mbaraka Kambona
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria imeiagiza Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) kwa kushirikiana na Taasisi ya Haki Maendeleo kuandaa
mapendekezo yatakayosaidia kuanzishwa kwa mchakato wa kutungwa kwa sheria ya kulinda haki za mtumiaji wa huduma za mifumo ya kimtandao na kuyawasilisha kwa kamati hiyo ili waweze kushawishi bunge na mamlaka nyingine husika ili sheria hiyo iweze kutungwa.
Maelekezo hayo yalitolewa na Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria, Emmanuel Mwakasaka, Mbunge wa Tabora Mjini kufuatia mada kuhusu
haki za binadamu na Mitandao iliyowasilishwa vyema na Mwenyekiti wa Bodi ya Haki Maendeleo, Dk. Abdallah Mrindoko katika warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kwa kushirikiana na Taasisi ya Haki Maendeleo kwa wabunge wa kamati hiyo Iliyofanyika Mkoani Morogoro Machi 16, 2020.
Akiongea baada ya kuwasilishwa kwa mada hiyo, Mwakasaka alisema kuwa kuna haja ya kuwa na sheria itakayolinda usiri wa taarifa za mtumiaji wa huduma zinazotumia mifumo ya
kimtandao kwa kuzingatia kuwa mifumo hii inachakata taarifa za mtumiaji na kuzisambaza jambo ambalo linaibua haja ya kutungwa kwa sheria hiyo.
Mapema wakati akitoa mada hiyo, Dk. Mrindoko alitaja changamoto kubwa inayowakumba watumiaji katika kipindi hiki cha maendeleo ya teknolojia ya mtandao ni uwepo wa taasisi nyingi zinazojihusisha na utunzaji na uchakataji wa taarifa katika mfumo wa kidijitali bila kuwepo na sheria ya kulinda haki hizo za mtumiaji.
Dk. Mrindoko aliongeza kuwa ili thamani ya matumizi ya mitandao iweze kutambulika vizuri ni muhimu kuwa na sera na sheria itakayosimamia ulinzi wa haki za mtumiaji nchini.
Aliendelea kusisitiza kwamba mapinduzi ya huduma ya kifedha kwa njia ya mitandao ya simu imeibua changamoto nyingi zinazohusiana na ulinzi wa haki za mtumiaji, akisema kuwa jukwaa hili limeleteleza muingiliano kati ya kampuni za mawasiliano na taasisi za kifedha, mazingira ambayo yameibua hoja ya kuwepo sheria ya kusimamia masuala hayo.
“Mazingira yaliyopo sasa yametengeneza ombwe la kisheria kufuatia kuwepo kwa pande mbili ambazo ni kampuni za simu na taasisi za kifedha zinazosimamia masuala ya kifedha
mitandaoni ambapo kila mmoja ana mipaka yake kiutendaji”, alisema Dk Mrindoko “Wakati matumizi ya simu katika kutuma na kupokea pesa kumepelekea ukuaji na urahisi wa
mzunguko wa masuala ya kifedha, bado kuna changamoto nyingi zinazohusu mustakabali wa mtumiaji ambazo zinahitaji kupatiwa ufumbuzi, aliongeza Dk. Mrindoko
Aidha, alieleza kuwa maendeleo katika matibabu ya afya ya kimtandao na kitambulisho cha uraia vimeleteleza maswali mengi kuhusiana na ulinzi na usiri wa taarifa za mtumiaji,
akipendekeza kuwa mambo yote haya inabidi yawe katika mfumo mmoja ambao utalinda usiri na taarifa za mtumiaji.
Akichangia majadiliano katika warsha hiyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Profesa Sifuni Mchome alikiri kuwa ni muhimu kuwa na sheria zinazolinda usiri na taarifa za
mtumiaji huku akisema kuwa mchakato wa kutunga sheria hiyo hivi sasa ipo katika mchakato
wa kutungwa ili iweze kutumika.
---Mwisho---
MAELEZO YA PICHA
PICHA NAMBA 7128
Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Dk Augustine Mahiga na Katibu wa Wizara hiyo, Profesa Sifuni
Mchome wakimsalimia Mbunge wa Malindi, Ally Saleh walipokutana Mkoani Morogoro kuhudhuria
warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) kwa
kushirikiana na taasisi ya Haki Maendeleo.
PICHA NAMBA 7163
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Jaji (Mst.) Mathew Mwaimu
akiwasilisha taarifa ya THBUB kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria katika warsha
iliyoandaliwa Mkoani Morogoro na THBUB kwa kushirikiana na Haki Maendeleo . Katikati ni
Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Emmanuel Mwakasaka, wa kwanza kushoto ni Waziri wa Katiba
na Sheria, Balozi Dk Augustine Mahiga.
PICHA NAMBA 7239
Kaimu Katibu Mtendaji wa THBUB, Hajjat Fatuma Muya akisisitiza jambo kwa Kamati ya Kudumu
ya Bunge ya Katiba na Sheria waliohudhuria warsha warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Tume ya
Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) kwa kushirikiana na taasisi ya Haki Maendeleo
Mkoani Morogoro jana.
PICHA NAMBA 7276
Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Dk Augustine Mahiga akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa
Taasisi ya Haki Maendeleo, Wilfred Warioba walipokutana Mkoani Morogoro katika warsha ya siku
moja iliyoandaliwa kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria. Warsha hiyo iliandaliwa
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) kwa kushirikiana na taasisi ya Haki
Maendeleo.
No comments:
Post a Comment