Mkurugenzi Mkuu wa AFRICAB Mansoor Moiz.
Na Mwandishi Wetu
UWEPO wa biashara ya mabomba ya plastiki (PVC)
yasiyo na ubora katika soko nchini kwa kiasi kikubwa kumetajwa kuchangiwa
na baadhi ya wenye viwanda
vinavyozalisha bidhaa hiyo kutozingatia sheria sambamba na waagizaji wasio wa
nje ya nchi wasio waaminifu.
Hatua hiyo
pamoja na mambo mengine imebainishwa
kuwa moja ya sababu kuu ya wananchi kupata hasara mbalimbali hususani pale
linapotokea bomba hilo kupasuka na kusababisha athari katika njia za umeme na wakati mwingine hata kusababisha
kuungua kwa nyumba na miundombinu
mingine ya umeme.
Kimsingi
mabomba hayo(PVC), huzalishwa maalumu kwa ajili ya matumizi ya usafirishaji wa
nyaya za umeme katika ujenzi wa nyumba
na majengo mengine lakini pia miundombinu inayotekelezwa katika miradi mbalimbali
ikiwemo ya majengo na umeme nchini.
Hayo
yamebainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha utengenezaji wa vifaa vya umeme
cha Kilimanjaro Cables (AFRICAB) kinachozalisha mabomba ya PVC maalumu kwa
ajili ya usambazaji wa umeme Mansoor Moiz, alipokuwa akizungumza na waandishi
wa habari jijini Dar es Salaam jana kuhusiana na uzalishaji wa bidhaa hizo
wanaoufanya
Kwa mujibu
wa Mansoor, Tanzania inapiga hatua kubwa
katika uzalishaji wa mabomba hayo, isipokuwa kumekuwepo na changamoto ya baadhi
ya wenye viwanda hivyo kuzalisha bidhaa zisizo na ubora.
Alisema
uzalishwaji huo wa mabomba yasiyo na ubora unaotakiwa kulingana na viwango vya
TBS, kimsingi umekuwa ukisababisha
athari katika soko na kwamba imekuwa ngumu kuwabaini wahusika wa bidhaa hizo kwa kuwa hawajitambulishi
katika bidhaa hizo kama watengenezaji.
“Kujenga
jina ya kampuni inachukua maisha lakini kwa mara moja unaweza kuanguka,
tunapaswa kuzingatia ubora wa bidhaa
zetu kulingana na matakwa ya Shirika la
Viwango Tanzania(TBS),ni wajibu wetu kuwa waminifu kwa Serikali yetu, kama wazalishaji wote tujifanya hivyo wazi
kuwa tutaepusha athari kwa
watanzania wenzetu ikiwemo kuokoa nyumba zao kuungua, fedha na hata
maisha yao kwa ujumla” alisema Mansoor
Alisema
kimsingi kazi ya usambazaji wa nyaya ‘cables’
maeneo tofauti ikiwemo chini ya ardhi inahitaji
mabomba yenye viwango vya
kutosha na teknolojia ya hali ya juu,
tofauti na hivyo mabomba hayo yanaweza
kupasuka na kusababisha madhara yasiyo tarajiwa huku akiwataka wenye viwanda
vinavyozalisha bidhaa hiyo nchini kote kuifanya kazi hiyo kwa ushirikiano wa
pamoja na weledi .
“Ni muhimu
tushirikiane kwa pamoja katika suala hili, tujivunie nchi yetu na viwanda vyetu
huku tukijua kuwa kuzalisha bidhaa zisizo na ubora ni kuwaumiza wananchi
wenzetu na kulikosea heshima taifa letu
ambalo katika uongozi huu chini ya Rais John Magufuli limetupa fursa kubwa ya kuwekeza katika viwanda” aliongeza Mansoor
Hivi
karibuni Rais John Magufuli alitoa rai
kwa wenye viwanda hao kuhakikisha wanazalisha bidhaa zenye ubora pamoja na
kuangalia uwezekano wa kuwa na bei ya chini ya bidhaa hizo ili kulinda soko la
ndani sambamba na kumwezesha mwananchi kumudu.
Alisema ni
ajabu kwa bidhaa zinazozalishwa hapa nchini kuwa na bei ya ghali zaidi ya zile
zinazoingizwa kutoka nje ya nchi na kuhoji nini sababu ya viwanda hivyo kuwa na
bei ya juu katika bidhaa hizo wakati hazilazikiki kusafirishwa kutoka nje ya
nchi.
No comments:
Post a Comment