Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, amesema kuwa Vyombo vya Ulinzi na Usalama Nchini vimejipanga vyema kuhakikisha vinadhibiti vitendo vya uhalifu hasa kutokana na vitendo vya vurugu vinavyoendelea katika nchi jirani ya Msumbiji.
Aidha, IGP Sirro, amewataka Watanzaania hususan vijana kuacha kutumiwa na watu wachache wanaowataka wajiingize kwenye vitendo vya uvunjifu wa amani nchini ikiwemo kufanya uhalifu.
IGP Sirro amesema hayo leo wakati akizungumza na baadhi ya wakazi wa eneo la Mnazi Mmoja mkoani Lindi, nakuwataka wananchi hao
wajikite katika shughuli halali za kujiletea maendeleo.
No comments:
Post a Comment