HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 08, 2020

ALIYEJIUNGANISHIA CHANNEL ZA DSTV AHUKUMIWA MIAKA MITATU

Na Mwandishi Wetu- Mwanza

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mwanza imemhukumu Adhabu ya kulipa faini ya Sh. 500,000 au kwenda jela miaka mitatu mmiliki wa Mtandao wa TV  Yusuf Kassim Feruzi  baada ya kumkuta na hatia ya kutenda kosa la kujiunganishia kinyemela channel 24 za  DSTV  ikiwemo  mechi za Ligi ya Uingereza (EPL)  bila kupata kibali cha kampuni ya Multi Choice Africa Ltd.

Hakimu Mkazi Boniface Lema akisoma hukumu hiyo alisema katika kesi hiyo ya jinai namba 373/2018, mshitakiwa alikuwa akikabiliwa na jumla ya makosa mawili. Kosa la kwanza ni kukiuka Haki Miliki chini ya  kifungu  cha 34(1)(a) ,(b) na kifungu Cha 42 (1) Cha  Sheria ya Haki Miliki ya mwaka 1999 Kama ilivyorejewa mwaka 2002.

Hakimu Lema alilitaja kosa la pili ni kuvunja haki Miliki   kinyume na kifungu Cha 24(1),(2) Cha Sheria ya Mtandao ya mwaka 2015.

"Baada ya kupitia ushahidi wa mashahidi Saba walioletwa na upande wa Jamhuri ...Mahakama imemtia hatiani mshitakiwa katika kosa la kwanza kwa sababu upande wa Jamhuri ndio wameweza kuthibitisha kosa pasi na shaka, na mahakama imemuachia huru kwa kosa la pili kwa sababu upande wa Jamhuri umeshindwa kuthibitisha  kosa...hivyo katika kosa la kwanza mshitakiwa atatakiwa alipe faini ya Sh 500,000 au kwenda jela miaka mitatu ili iwe funzo kwa wengine" alisema Hakimu Lema.

Awali Wakili wa Serikali  Sabina CHOGHORHWE na Lilian Meli  walidai  mahakamani hapo  kuwa Novemba 19 mwaka 2016 eneo la Ghana Karume ,Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza mshitakiwa huyo ambaye Ni mfanyabiashara kwa njia ya udanganyifu akifanyabiashara ya kuonyesha mechi za Ligi ya Uingereza na alitumia jumla ya channel 24 kupitia  Ghana  Tv Network  bila kibali cha  Multi Choice  Tanzania Ltd ambao ndio wamiliki wa Haki Miliki hiyo kwa hapa nchini kwa niaba ya Multchoice  Africa Ltd.

CHANZO: Gazeti la Mtanzania. 8/4/2020.

No comments:

Post a Comment

Pages