Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza, akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa Benchmark Production Madam Ritha Paulsen kuhakikisha ndani ya mwezi mmoja anamlipa mshindi wa kwanza wa mashindano hayo Bongo Star Search wa mwaka 2019 Bw.Meshack Fukuta, mbele ya
waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Aprili 08,202 Jijini Dodoma, na kulia ni mshindi wa kwanza wa Shindano la Bongo Star Search mwaka 2019 (BSS) Bw.Meshack Fukuta.
waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Aprili 08,202 Jijini Dodoma, na kulia ni mshindi wa kwanza wa Shindano la Bongo Star Search mwaka 2019 (BSS) Bw.Meshack Fukuta.
Mshindi wa kwanza wa shindano la Bongo Star Search (BSS) la mwaka 2019 yanayoendeshwa na Kampuni ya Benchmark Production, Meshack Fukuta, akitoa
ufafanuzi kuhusu kiasi cha pesa alicholipwa kama zawadi aliyoahidiwa kuwa ni Sh. Milioni moja na siyo milioni mbili kama inavyoelezwa katika mkutano wa Naibu Waziri
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza na waandishi wa habari (hawapo pichani).
ufafanuzi kuhusu kiasi cha pesa alicholipwa kama zawadi aliyoahidiwa kuwa ni Sh. Milioni moja na siyo milioni mbili kama inavyoelezwa katika mkutano wa Naibu Waziri
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza na waandishi wa habari (hawapo pichani).
Baadhi ya waaandishi wa Habari wakifuatilia maelekezo ya Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza kwa Mkurugenzi wa Benchmark Production Madam Ritha Paulsen (hayupo pichani) kuhakikisha ndani ya mwezi mmoja anampatia mshindi wa kwanza wa mashindano Bongo Star Search ya mwaka 2019 zawadi yake ya milioni 50 leo Aprili 08, 2020 Jijini Dodoma.
Na Shamimu Nyaki – WHUSM, Dodoma
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza ametoa mwezi mmoja kuanzia Aprili 08, 2020 kwa Kampuni ya Benchmark Production inayoendesha mashindano ya Bongo Star Search chini ya Mkurugenzi wake Madam Ritha Paulsen kumlipa kiasi cha Shilingi milioni 50 mshindi wa kwanza wa mashindano hayo kwa mwaka 2019, Meshack Fukuta.
Naibu Waziri ametoa maelekezo hayo leo Jijini Dodoma baada ya kupokea barua kutoka kwa familia ya mshindi huyo iliyoeleza kutokutekelezwa kwa ahadi hiyo kwa takriban miezi minne sasa ilioanisha utaratibu wa malipo hayo kuwa milioni 30 ni kwa ajili kutengeneza kazi za muziki na matangazo kwa kipindi cha mwaka mmoja na milioni 20 ni ya kukabidhiwa mkononi ambapo Naibu Waziri amesisitiza
makubaliano yote yalioanishwa kufanyiwa kazi.
“Mimi kama mlezi wa tasnia ya Sanaa ambaye pia nilikua mgeni rasmi siku ya fainali nimesikitishwa sana na malalamiko haya, hivyo naitaka kampuni ya Benchmark kutekeleza ahadi hiyo na wasipofanya hivyo ndani ya muda huo, Serikali haitasita kufungia mashindano hayo”, alisema Shonza.
Naibu Waziri ameongeza kuwa Wizara iliwasiliana na uongozi wa Benchmark kuhusu malalamiko hayo mbapo Kampuni hiyo ilieleza kuwa imeshindwa kumlipa msanii huyo kutokana na viongozi wa Kampuni iliyodhamini shindano hilo ya Startimes kuwepo nchini China na kushindwa kusafiri kuja nchini kutokana na uwepo wa
ugonjwa wa Corona.
ugonjwa wa Corona.
Hata hivyo Naibu Waziri ameleeza kuwa Wizara iliwasiliana na uongozi wa Startimes ambao umekiri kuwa umeshalipa fedha kwa Kampuni ya Benchmark tangu
mwezi Januari 2020.
Aidha, Shonza ameitaka kampuni hiyo kuhakikisha inamtengenezea msanii huyo wimbo bora pamoja na kuufanyia matangazo ya kutosha katika kipindi cha miezi
miwili kuanzia leo pamoja na kuwasilisha nakala ya mkataba wa washiriki waliofikia hatua ya kumi bora ndani ya wiki moja kuanzia leo machi 08,2020.
Katika hatua nyingine Shonza ameliagiza Baraza la Sanaa na Taifa (BASATA) kusimamia utaratibu wa uaandaji wa mashindano mbalimbali ikiwemo kuwepo kwa
mikataba kati ya wasanii na wanaondesha mashindano au shughuli yoyote ya sanaa na wasanii pamoja na kuhakikisha ahadi wanazopewa washindi ikiwemo zawadi zinakuwepo na zinakabidhiwa kwa wahusika mara baada ya mashindano.
Kwa upande wake Meshack Fukuta mshindi wa shindano hilo kwa mwaka 2019 ameishukuru Serikali kwa namna ambavyo imechukua hatua katika malalamiko yake
ambapo ameahidi kufanya juhudi katika Sanaa yake ili kuitangaza nchi vizuri ndani na nje ya nchi pamoja na kujipatia kipato kupitia kipaji hicho.
No comments:
Post a Comment