HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 18, 2020

ASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KUINGIZA SUKARI YA MAGENDO

 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi (ACP) Blasius Chatanda, akizungumza na waandishi wa habari ambao hawapo pichani kuhusu operesheni walioiendesha ya kupambana na biashara haramu za magendo.
Sehemu ya waandishi wa habari Jijini Tanga wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye mkutano huo.


Na Mwandishi Wetu, Tanga
 
JESHI la Polisi Mkoani Tanga linamshikilia mkazi wa Kijiji cha Kigombe Kata ya Kigombe wilayani Muheza mkoani Tanga ambaye aliyeshirikiana na wenzake ambao walikimbia wakiwa wameingiza bidhaa za magendo kutoka nchini India kwa kutumia bandari Bubu ya Kigombe.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi (ACP) Blasius Chatanda alisema kwamba hatua ya kukamatwa kwa mkazi huyo ni kutokana na operesheni zinazoendelea kufanywa na Jeshi la Polisi kuhakikisha wanazibiti biashara za magendo.

Alisema kwamba tukio hilo lilitokea Aprili 17 Saa tisa mchana kwenye maeneo ya Mwarongo Kata ya Marungu Tarafa ya Pongwe ambapo wakiwa kwenye operesheni hiyo walifanikiwa kumkamata mtu huyo akiwa na mifuko 88 ya sukari yenye kg 50 ambayo imeonekana kutenegenezwa nchini India ikiwa inaingizwa nchini kwa njia za magendo.

Kamanda huyo alitaja bidhaa nyengine ambazo zilikamatwa kuwa ni Madumu 45 ya Oili ya Magari yenye kg 20 kila mmoja na mifuko mitano ya mchele yeye ujazo wa kg 50 kila mmoja ikitokea nchini Pakistani.

Kamanda Chatanda alimtaja mtuhumiwa ambaye alikamatwa kuwa ni Hassani Tausilo aliyeshirikiana huku wenzake ambao alikuwa akishirikiana nao kukimbia na kutokomea kusikojulikana ambao kwa sasa bado wanasakatwa na jeshi hilo kutokana na kufanya biashara haramu ya magendo

“Sehemu ya sukari ilikamatwa inasafirishwa kwenye pikipiki tayari ilishashuhwa kwenye Ngalawa na kwenda kufichwa kwenye mapori yaliyopo kwenye kijiji cha Kigombe na kuanza kusafrisjwa kwa kutumia pikipiki ambazo pia nazo tulifanikiwa kuzikamata na mpaka sasa tunazishikia”Alisema kamanda huyo.

Aidha alisema hivi sasa wanachoendelea nacho ni msako ulioanza kwenye mapori na kufanikiwa kukamatwa mifuko mengine 78 baada ya mifuko 10 kukamatwa kwenye pikipiki na mtuhumiw aliyekuwa kwenye pikipiki hiyo naye alikimbia huku pia na mafumu 45 na huo mchele.

Hata hivyo Kamanda huyo alitoa wito kwa wafanyabiashara watambue kwamba biashara ya magendo sio biashara tena na itawaingiza kwenye umaskini hivyo waachane nayo huku akisisitiza kwamba operesheni hiyo ni endelevu na kamwe haitawapa nafasi na kila anakayejiingia atambua kwamba kwenye biashara hiyo atambua kwamba atakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya dola.

No comments:

Post a Comment

Pages