Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akiteta na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, Bungeni jijini Dodoma leo Aprili 30, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
NA WAMJW Dodoma
Wizara ya Afya, kupitia Idara kuu ya
Maendeleo ya Jamii inatarajia kutumia Jumla ya shilingi bilioni 33.195 ili kutekeleza
shughuli mbalimbali za kijamii hususani zilizopewa kipaumbele kwa mwaka wa
fedha 2020/21.
Akiwasilisha
Hotuba ya Wizara ya
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy
Mwalimu amesema katika mwaka wa fedha 2020/21 Idara Kuu ya
Maendeleo ya Jamii inatarajia kutumia kiasi hicho cha fedha kwa lengo la
kuimarisha huduma na mafunzo kwenye Taasisi za Ustawi na Maendeleo ya
Jamii,
kukarabati makazi ya wazee, kujenga mahubusu za watoto na kutokomeza
ukatili wa
kijinsia.
Alisema kuwa bajeti hiyo itasaidia
kuimarisha Kujenga kumbi pacha na hosteli katika Taasisi ya Maendeleo ya Jamii
Tengeru ambapo jumla ya shilingi bilioni 2.7 zimetengwa, pia
kuboresha utoaji wa mafunzo ya taaluma ya maendeleo ya jamii ili kukidhi
mahitaji ya soko sambamba na kukuza ujuzi wa wahitimu ikiwemo kuwajengea uwezo
wa kujiajiri na kuajiriwa kwa kutenga jumla ya shilingi bilioni 6.6.
Maeneo mengine yaliyotengewa fedha
ni pamoja na ukarabati wa majengo na miundombinu katika makazi ya wazee
kwa shilingi milioni 400, ujenzi wa Shule ya Maadilisho katika Mkoa
wa Geita shilingi milioni 200, kuimarisha ujenzi wa mahabusu ya
watoto katika mikoa ya Kigoma na Mtwara shilingi milioni 700 na
kuwezesha Taasisi ya Ustawi wa Jamii kuboresha utoaji wa mafunzo yanayokidhi
mahitaji ya soko shilingi milioni 250.
Aidha, jumla ya shilingi milioni
827.95 zimetengwa kwa ajili ya shughuli za kutokomeza ukatili wa kijinsia
katika jamii.
“Ili kutekeleza vipaumbele
vilivyoanishwa kwa mwaka 2020/21, Wizara kupitia Idara kuu ya Maendeleo ya
Jamii imekadiria kutumia kiasi cha shilingi bilioni 33 kwa
ajili ya kutekeleza majukumu mbalimbali ya Wizara ikiwa ni pamoja na uendeshaji
wa ofisi na miradi ya maendeleo” alisema.
Mhe. Ummy amesema Wizara imeendelea
kukuza ari ya jamii kushiriki katika kujiletea maendeleo ya kijamii na kiuchumi
kwa kutumia nguvu kazi na rasilimali zinazowazunguka na kusimamia masuala yote
ya ushirikishwaji wa jamii kwenye sekta mbalimbali.
No comments:
Post a Comment