Wananchi waliokuwa wakichimba mchanga katika mto salasala.
Meneja wa TARURA wa
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Mhandisi Leopold Runji akitoa maelezo kwa kuu mwa Wilaya hiyo, Daniel Chongolo kuhusu miundombinu ya barabara katika
makazi ya TBA muda mfupi baada ya kutoka kukagua mito inayochimbwa mchanga.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Daniel Chongolo akiwa na wajumbe wa kamati
ya ulinzi na usalama wa Wilaya walipofika kwenye mto salsala na kukutana na
watu wakikimbia na chepe mara baada ya kuona msafara huo.
Dar es Salaam, Tanzania
Mkuu wa
Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo, ameliagiza Jeshi la Polisi Wilayani
hapo kuwachukulia hatua wale wote watakaobainika kuingia kwenyemito na kuchimba
mchanga katika bonde la mto Salasala, bonde la mto Mbezi na bonde la mto Tegemeta.
Chongolo ametoa agizo hilo leo wakati alipofanya ziara na wajumbe wa kamati ya
ulinzi na usalama ya wilaya na kushuhudia vitendo hivyo vikiendelea ikiwa ni takribani
miezi miwili imepita tangu kuendesha zoezi la upandaji miti ya mianzi na magugu
pamoja na kusitishwa kwa vibali vya uchimbaji wa mchanga viliyotolewa na Bodi ya Maji Bonde la
Ruvu.
Amesema kuwa
licha ya kutoa maelekezo pamoja na kusitishwa kwa vibali hivyo lakini bado wananchi
wanaendelea kuchimba mchanga jambo ambalo amesema linahatarisha nyumba za
makazi ya watu na hivyo kulisisitizia jeshi hilo kuwachukulia hatua wananchi
hao ambao wanajihusisha na shuguli hizo.
“Tulishazuia
hii mito isichimbwe mchanga, tumepita
mto Salasala, Mbezi kule kwenye daraja la Malechela, pamoja na huku juu mpakani
mwa eneo la jeshi la Lugalo, bado vitendo hivi vinaendelea nasisitiza
naninaagiza jeshi la polisi kwenye Wilaya ya Mabwepande na Kawe ambayo ndio
inahusika, niliagiza na leo narudia kwa mara ya pili hatutakuwa na msamaha
kwenye jambo hili.
Amefafanua kuwa
“mtu yeyote ambaye ataonekana analea vitendo vya uharibifu huu wa mazingira, tukimkuta na kumkamata tutamchukulia hatua
kali za kisheria kwasababu jukumu letu sisi viongozi ni kusimamia na kuilinda sheria.
Chongolo amesisitiza kuwa“ Hatuko hapa kuwaonea watu, wala kuwaacha wananchi waharibikiwe na nyumba zao
kwasababu ya maslahi na uroho wa watu wachache, kufanya hivi ni kuhujumu maslahi
ya nchi hatuwezi kuendelea kuwaacha watu wanamna hii kwa hiyo nilazima tuchukue
hatua kwa kila tutakaye mbaini anafanya shughuli hii.
Aidha Chongolo amesema kuwa baada ya ziara hiyo ataunda timu ya kufuatilia mwenendo
wa watu hao kwa kuwa alishatoa maagizo ya kuwashugulikia wote wanaohusika na
kufanya shuguli za kuchimba mchanga kwenye mito hiyo.
Mapema mwaka
huu, Chongolo alisitisha vibali vya uchimbaji mchanga vilivyotolewa na Bodi ya
Maji Bonde la Ruvu kutokana na kuleta madhara ya uharibifu wa mito na
kusababisha athari kwenye makazi ya watu katika Halmashauri hiyo.
Vibali
vilivyositishwa ni vile vilivyotolewa kufanya shughuli hizo katika Bonde
la mto Salasala, Mto mbezi, Ndumbwi, Nyakasangwe, na kusema kuwa mito hiyo
inapita katikati ya makazi ya watu na kwamba baada ya kufanyika marekebisho
utawekwa utaratibu upya wa kufanya shughuli hizo.
No comments:
Post a Comment