Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi
Paskasi Muragili akiwa ndani ya basi la Kampuni ya Kiazi Kitamu akiwaeleza
abiria mbinu za kujikinga na Virusi vya Corona (COVID-19) alipokuwa kwenye
Operesheni maalum ya Tokomeza Corona Katika Manispaa ya Singida kwenye Kituo
Kikuu cha mabasi.
1 Madereva na Mawakala wa mabasi kwenye
Kituo Kikuu cha mabasi ya Mkoa wa Singida (Misuna) wakionyesha jinsi ya kutumia
vitakasa mikono ili kukabiliana na ugonjwa wa Corona (COVID-19) kwa Mkuu wa Wilaya
ya Singida Mhandisi Paskasi Muragili (Hayupo pichani) alipofanya Operesheni Maalum
ya Tokomeza Corona Katika Manispaa ya Singida kuona utekelezaji wa maagizo ya
Serikali ya kujikinga na ugonjwa huo.
Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskasi
Muragili (aliyenyanyua mkono) akihoji uelewa wa kujikinga na virusi vya Corona
(Covid-19) mahali pa kazi kwenye maduka ya kuuzia nyama alipofanya Operesheni Maalum
ya Tokomeza Corona Katika Manispaa ya Singida kwenye Soko Kuu la Singida Mjini.
Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi
Paskasi Muragili akiwasisitiza wafanyabiashara wadogo juu ya matumizi sahihi ya
vitakasa mikono alipofanya Operesheni maalum ya Tokomeza Corona Katika Manispaa
ya Singida kwenye Soko Kuu la Singida Mjini. (Picha na Peter Kashindye).
No comments:
Post a Comment